Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV Hananga.
MBUNGE wa Jimbo la Simanjiro mkoani Manyara Christopher Ole Sendeka ameshauri kwamba ni vema wana CCM kuanzia ngazi ya Shina, Tawi, Kata, Wilaya na Mkoa wakajiimarisha kiuchumi ili kupata nafasi ya kuweka utaratibu wa kuwawezesha viongozi wakiwemo mabalozi katika maeneo yao.
Ametoa ushauri huo leo Machi 5,2023 mbele ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Daniel Chongolo ambaye ameanza ziara ya kikazi katika mkoa wa Manyara na baada ya kupokelewa akashiriki kikao cha Balozi wa Shina namba Sita katika Kata ya Hirbadaw wilayani Hanang mkoani hapa.
“Katibu Mkuu umenipa nafasi ya kuelezea hili la wajibu wa viongozi wetu , jambo la kwanza katika nafasi hii ya balozi na nianze kwa kukupongeza kuja kutoa nafasi maalum kwa balozi , nikukileta chama mikononi mwa wanachama katika uhalisia wake kwasababu ndio kazi ya msingi ya uongozi katika chama chetu.
“Na Kampeni hii umeiongoza wewe najua chini ya kampeni ya Rais Mama Samia Suluhu Hassan nakupongeza ndugu Katibu Mkuu.Sasa Chama chetu kina nafasi ya haki za za wanachama , kuna wajibu wa mwanachama .Chama hiki kimekuwa kikiendeshwa kwa watu kujitolea ili Chama kiweze kwenda mbele kwasababu ni chetu.
“Lakini niseme hili la sabuni ya mabalozi ,Chama kiliamua kutoa chochote kitu kidogo katika zile sabuni mwanzoni mwa wakati wa uchaguzi lakini Chama chetu ni kikubwa mno, Mashina tuliyonayo Mkoa wa Manyara ni 10,847 mkoa wa Manyara.Je kwa Tanzania zima tuna mashina mangapi? Ni mengi sana,”amesema Ole Sendeka.
Amefafanua hiyo maana yake ni kamba lazima wajitahidi katika ngazi zao za msingi kukubaliana na maelekezo ya Chama kwamba wajenge uchumi wa chama chao kutoka kwenye matawi, Shina,tawi, Kata , Wilaya na Mkoa ili kupanua wigo wa uchumi.
“Ukiimarisha Chama ngazi ya msingi mnaweza kuwa na utaratibu wenu wa kupatiana sabuni ninyi wenyewe katika maeneo hayo wakati Chama kinaendelea kujenga uwezo lakini uwezo wa Chama ngazi ya taifa unategemea uwezo unaojengwa huku chini. Kwa hiyo nilitaka niseme hayo kwa kifupi ndugu katibu mkuu sijajua kama nimekidhi lakini haya ndio maoni yangu.
“Tupate uwezo ambao unaweza kuwa na ziada ya kusema tutote sabuni kwa mabalozi wetu , kuna wajibu wa mwanachama na Chama na chama kimekuwa kikiendeshwa kwa watu kujitolea ili kiweze kwenda mbele kwani chama chetu.”
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo akimsikiliza MBUNGE wa Jimbo la Simanjiro mkoani Manyara Christopher Ole Sendeka alipokuwa amepewa nafasi ya kueleza kuhusu wajibu wa viongozi kuanzia ngazi ya Shina, Tawi, Kata, Wilaya na Mkoa aliposhiriki kikao cha balozi wa shina namba 6 katika Kata ya Hirbadaw wilayani Hanang
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...