Na.Mwandishi wetu, Arusha
Mkuu
wa mkoa wa Arusha ,John Mongela amezitaka taasisi mbalimbali
kuhakikisha kunakuwepo na uwiano sawa wa jinsia kati ya wanaume na
wanawake ili kuwepo kwa usawa mahala pa kazi.
Ameyasema hayo
jijini Arusha wakati akizungumza na wadau mbalimbali wa benki ya CRDB
walipokutana katika chakula cha jioni katika kilichokutanisha wanawake
wadau wa benki hiyo Jijini Arusha.
Mongela alisema kuwa,hakuna
agenda ya maendeleo inayoweza kufikiwa bila kukabiliana na changamoto
zinazowakabili wanawake na kuweza kupatiwa ufumbuzi kwani wanawake ni
jeshi kubwa na wana mchango mkubwa sana katika jamii.
"Naipongeza
sana benki ya CRDB kwa namna ambavyo imejitahidi kukumbatia usawa wa
kijinsia na kuweza kuwajengea uwezo wa kuwezesha wafanyakazi wa kike
kwani nameambiwa asilimia 47 ya wanawake ni wafanyakazi wa benki hii
huku wanaume wakiwa ni asilimia 53 na juhudi zaidi zinaendelea za
kuongeza idadi ya wanawake ni mfano mzuri wa kuigwa na taasisi zingine.
"amesema Mongela.
Kwa upande wake Afisa mkuu mwendeshaji wa
benki ya CRDB ,Bruce Bwile amesema kuwa,kumekuwepo na ongezeko la
asilimia 3 la idadi ya wanawake katika benki hiyo tofauti na miaka ya
nyuma na kuweza kuleta dhana nzima ya usawa wa kijinsia mahala pa
kazi.
Amesema kuwa, benki hiyo ina programu ya kuweza
kuwajengea uwezo wanawake katika ngazi ya kati ambapo wanawake mia moja
wanashiriki katika programu hiyo huku lengo kuu ni kufikia idadi zaidi
ya mia mbili ili kuleta usawa wa kijinsia.
"Kupitia kitengo
cha biashara benki imeweza kufikia wanawake wadogo na wa kati kwa kutoa
kiasi cha shs 67.3 bilioni hadi desemba 2022 ambapo jumla ya wanawake
3,122 wameweza kufikiwa katika mikoa yote Tanzania."amesema Bruce.
Aidha
amesema kuwa, benki hiyo imeendelea kusisitiza jitihada zake katika
maswala ya kijinsia na kukumbatia usawa katika jamii kwa ujumla ili
kuondokana na changamoto ya kupigania usawa mahala pa kazi penye
uwiano.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...