Na Mwamvua Mwinyi,Miono
Mbunge wa Jimbo la Chalinze ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti na Utumishi wa Umma Ridhiwani Kikwete, ameshiriki sherehe za kuwaaga wanafunzi wanaomaliza kidato cha 6 katika shule ya sekondari ya Kikaro Miono
Katika sherehe hizo , Ridhiwani aliwasisitizia wanafunzi hao kuepuka tamaa za dunia na kujali masomo kwanza.
Aidha Ridhiwani,amekabidhi msaada kutoka Serikali ya wanafunzi wa IFM kupitia kamati ya Charity 2023 ambao ni matundu 20 ya choo kwa ajili ya wanafunzi na walimu, taulo za kike katika shule ya Msingi Miono.
Pia baiskeli nne kwa ajili ya watoto wenye ulemavu, bima za afya kwa watoto 40 wenye mahitaji maalum katika kituo cha Hope disability centre.
Msaada huo umetolewa wakati IFM Charity inatimiza miaka 10 tokea wameanza kutoa msaada ambayo imeendana na maadhimisho ya miaka 10 ya IFM Charity.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...