Na Janeth Raphael - MichuziTv Dodoma
TANZANIA inaungana na Jumuiya ya Hali ya Hewa Duniani kuadhimisha siku ya hali ya hewa Duniani (WMD) kwa mwaka 2023.
Jumuiya ya Hali ya Hewa Duniani inatumia siku hii kuadhimisha siku ambayo mkataba wa kuanzishwa kwa Shirika la Hali ya Hewa Duniani ulisainiwa Machi, 2050.
Naibu waziri wa Ujenzi na Uchukuzi ( Sekta ya Uchukuzi) Atupele Mwakibete ameyaeleza hayo leo jijini Dodoma ambapo amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi 193 wanachana wa WMO na inaungana na Jumuiya ya Kimataifa kuadhimisha miaka 73 ya WMO na maadhimisho ya miaka 159 ya shirika la kwanza la Kimataifa la Hali ya Hewa.
Mwakibete amesema uchumi wa Tanzania unategemea sana Sekta zinazotegemeana na zinazoathiriwa na hali ya hewa na uoatikanaji wa rasilimali maji ambazo ni muhimu katika kupanga na kufanya maamuzi ambapo miongoni mwa Sekta hizo ni kilimo, mifugo, uvuvi, nishti na maji pia mfumo na mzunguko wa maji huchangia kutengeneza mvua ambayo tunategemea katika upatikanaji wa rasilimali maji.
" Utoaji wa huduma bora za hali ya hewa na maji umekuwa kipaumbele kwa Serikali ya Tanzania katika awamu zote, huduma hizi zina umuhimu mkubwa na kuongeza tija katika maendeleo ya sekta zote za kijamii na kiuchumi " - Amesema Mwakibete.
Katika kukabiliana na changamoto za athari za mabadiliko ya hali ya hewa kunahitajika jitihada na hatua za makusudi na endelevu ikiwa ni pamoja na kujenga Taasisi madhubuti kwa ajili ya kuboresha na kutoa huduma bora za hli ya hewa Nchini.
" Hii ni pamoja na kuongeza kiasi cha data za hali ya hewa tunazobadilishana na nchi nyingine kupitia mifumo maalumu ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani " - Mwakibete
Mwakibete amesema katika kuhakikisha kunakuwa na taarifa za uhakika za hali ya hewa Serikali ya Tanzania imefanya Uwekezaji mkubwa katika huduma za hali ya hewa Nchini ikiwemo ununuzi wa miundombinu ya kisasa ya uchunguzi wa hali ya hewa ikiwa ni pamoja na Rada za hali ya hewa.
"Tuna Rada saba ambapo Rada tatu zimeshasimikwa katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu, Rada mbili zimeshafika na tunategemea kuzifunga hivi karibuni katika Mkoa wa Mbeya na maeneo ya Kigoma na Rada mbili zipo kiwandani zinatengenezwa" - Mwakibete.
Aidha Mwakibete amesema Serikali itaendelea kushughulikia mapungufu na mahitaji yanayohusu utoaji huduma za hali ya hewa Nchini kwa nia ya kuboresha huduma za tahathari zinazoendana na kasi na kukabiliana na maendeleo ya Kimataifa ya sayansi na Teknolojia pamoja na kuunga mkono Mpango wa Umoja wa Mataifa wa kuhakikisha kuwa tahathari za hali ya hewa zinawafikia watu wote Duniani.
Hata hivyo Mwakibete ametoa wito kwa wadau wote kutumia vyema taarifa za hali ya hewa zinazotolewa na Mamlaka ya hali ya hewa Nchini kwa ajili ya kupanga shughuli za kijamii na kiuchumi na kufanya maamuzi ya pamoja na kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na tabia nchi.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini Dkt Ladislaus Chang'a amesema katika ukanda wa Afrika Mashariki na Dunia nzima kuna changamoto ya mabadiliko ya hali ya hewa ambayo yanapelekea kubadilika kwa misimu ya mvua na upunguaji wa kunyesha mvua.
"Tunatarajia mvua zitaendelea kuwa za wasitani katika maeneo mengi nchini hivyo tunawasisitiza wakulima kuzingatia ushauri wa kitaalam kutoka kwq maafisa Ugani ambao wanaweza kutafsiri vizuri taarifa hizi pamoja na kupanda mazao yanayokomaa haraka na yanayostahimili hali ya ukame." - Dkt Chang'a
NAIBU Waziri wa ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi) Atupele Mwakibete akizungumza na (wanahabari hawapo pichani) ikiwa ni maadhimisho ya siku ya hali ya hewa Duniani leo jijini Dodoma.
KAIMU Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Dkt Ladislaus Chang'a akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) ikiwa leo ni siku ya maadhimisho ya hali ya hewa Duniani Jijini Dodoma.
KAIMU Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Dkt Ladislaus Chang'a akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) ikiwa leo ni siku ya maadhimisho ya hali ya hewa Duniani Jijini Dodoma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...