Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
Wekundu
wa Msimbazi, Simba SC wamefanikiwa kukwea hadi nafasi ya pili katika
Kundi C la Michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika (CAF CL) baada ya
kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Vipers SC ya Uganda kwenye uwanja wa
Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Katika mchezo huo wa nne wa
Kundi hilo C, Wekundu wa Msimbazi walianza vyema mchezo huo kuwasakama
Cobra wa Uganda, ambapo dakika ya 45+1’ Kiungo Mshambuliaji, Clatous
Chama alipachika bao hilo pekee baada ya kuwadanganya Walinzi wa Vipers
SC na kupiga ‘shuti’ kali lililompita Golikipa Alfred Mukereza.
Kwa
matokeo hayo, Simba SC wamefufua matumaini makubwa ya kufuzu hatua ya
Robo Fainali ya Michuano hiyo baada ya kufikisha alama sita katika Kundi
hilo lenye timu za Raja Casablanca ya Morocco, Horoya AC ya Guinea na
Vipers SC.
Raja AC wanaendelea kuongoza Kundi wakiwa na alama 12
huku Simba SC wakiwa nafasi ya pili wakiwa na alama sita, Horoya AC wana
alama nne huku Vipers wakiwa na alama moja pekee.
Machi 18, 2023
Simba SC watakuwa na kibarua dhidi ya Horoya AC kwenye uwanja wa
nyumbani wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, huku Raja Casablanca watakuwa
ugenini dhidi ya wenyeji Vipers SC kwenye dimba la St. Mary’s, Kitende
mjini Entebbe nchini Uganda.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...