Spika wa Bunge la Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kundi la Afrika katika Umoja wa Mabunge Duniani (Africa Geopolitical Group in the IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson, leo Machi 12, 2023 amehutubia Mkutano wa 146 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) unaoendelea Nchini Bahrain wakati Kauli mbiu mkutano huo ni “Kukuza amani na kujenga Jamii Jumuishi yenye kuvumiliana”.
Dkt. Tulia amezungumzia kuhusu kuhusu juhudi zinazofanywa na Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Bunge katika kudumisha amani na mahusiano mazuri ya kijamii kwa Wananchi wake pamoja na kuheshimu Maazimio ya Kimataifa katika kulinda na kudumisha amani Duniani.
Wakati huohuo, Dkt. Tulia amewasilisha hoja ya dharura kwa niaba ya kundi hilo kuchagiza kuundwa kwa mfuko wa maafa Duniani kwa ajili ya kusaidia Nchi zinazoathiriwa na majanga ya asili na mabadiliko ya tabianchi.
Pamoja na hoja hii, hoja zingine nne ziliwasilishwa na Mataifa mbalimbali. Hoja hizi zinatarajiwa kupigiwa kura ya maamuzi hapo baadae ili Umoja huo kupitisha hoja moja ya dharura ambayo itajadiliwa, kuboreshwa na hatimaye kutengeneza azimio la Mkutano huo.
Spika wa Bunge la Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kundi la Afrika katika Umoja wa Mabunge Duniani (Africa Geopolitical Group in the IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiteta jambo na Mhe. Ester Matiko ambaye ni Mbunge wa Tanzania anayewakilisha Umoja huo wa IPU wakati wa Mkutano wa 146 unaoendelea Manama Nchini Bahrain.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...