WAFANYAKAZI 21 wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Yohana (St. John's University of Tanzania) wakiwemo maaskofu, mapadri na madaktari wamefungua kesi Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) kwa sababu ya kuachishwa kazi bila utaratibu kufuatwa. 


Amina Sangali na wenzake 20 walifikia uamuzi huo, baada ya chuo hicho kufunga tawi lake lilipo Buguruni Malapa, jijini Dar es Salaam ambalo lilikuwa ni Chuo cha Mapadri (St. Mark's) bila kuwapa barua za kuwaachisha kazi. 

Katika hati yao iliyowasilishwa katika tume hiyo na Wakili Sylivatus Mayenga wafanyakazi hao wanaiomba time ione utaratibu wa kufukuzwa kazi haukuwa sawa, kwa sababu chuo kimefungwa lakini hawajawahi kupewa barua ya kuonesha ukomo wa ajira zao. 

Pia, wafanyakazi hao wanaomba tume ione kuwa wamejengewa mazingira magumu ya kazi, kwa sababu ya kushindwa kupatiwa kazi za kufanya na kutokulipwa mishahara yao na malupulupu na stahiki zingine. 

Novemba 5,2019 baada ya chuo kufungwa  wafanyakazi 31 wa tawi hilo walipeleka malalamiko yao ya kutolipwa mishahara yao kwa Afisa Kazi Mfawidhi wa Dar es Salaam, ambapo akatoa uamuzi kwamba mwajili (St. John's) 
anatakiwa kuwalipa mishahara yao. 

Hata hivyo, Chuo hicho hakikubaliana na uamuzi huo uliyotolewa Mei 27,2020 na Yusuph Nzugile, kilikata rufaa kwa Kamishina wa Kazi, Ristone Malingumu, lakini Kamishna huyo aliendelea kusimamia uamuzi wa Afisa Kazi kuwa walipwe mishahara yao. 

Baada ya uamuzi huo wa Maliamungu alioutoa Julai 24,2020, Kamishna huyo alipeleka kikazia hukumu mbele ya Msajili wa Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi, Sundi Fimbo dhidi ya St. John's Septemba 6,2022.

Wakati hatua hiyo inaendelea, St. John's walifungua maombi katika Mahakama hiyo mbele ya Jaji Magimbi dhidi ya St. Mark's na wafanyakazi wakipinga kuwa sio wafanyakazi wao na kwamba suala lililokuwa mbele ya Msajili lisimame hadi kesi hiyo itakaposikilizwa na kutolewa uamuzi. 

Katika uamuzi wake, Jaji Magimbi alitupilia mbali maombi hayo na ile hatua ya kukazia hukumu iliyokuwa kwa Msajili ikaendelea, lakini baada ya muda kidogo St. John's wakaomba wafanyakazi hao wakubaliane nje ya mahakama. 

Waliingia makubaliano hayo na ya kuyapeleka mbele ya Msajili kwa sababu tayari kulikuwa na kesi yakasajiliwa mahakamani hapo, ambapo St. John's ilikubaliana na wafakazi hao kuwalipa mishahara yao kwa awamu tatu. 

St. John's walitekeleza makubaliano hayo kwa awamu mbili, ambapo awamu yatatu ambayo ilitakiwa itekelezwe Februari 28,2023 haijatekelezwa ambapo ni madai ya zaidi ya sh. milioni 200.

Mbali na Sangali wengine ni Askofu Emmaus Mwamakula, Msaidizi wa Askofu wa Mashiriki na Pwani (Anglikana), Richard Kamenya, Kiongozi wa Kanisa la SMC, Patri Lukas Saidi, Kiongozi wa Kanisa la Anglikana Mbweni. 

Mapadri wengine ni Emmanuel Saninga, Yohana Mtokambali na Samwel Lipembe pia katika madai hayo kuna madaktari ambao ni Dk Anna Ndebukwa na Dk Beatrice Halii, Noela Kawia, Michael John, Sophia Msangi, Chard Daniel na wengine nane.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...