Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Kamishna msaidizi wa Polisi Allan Bukumbi _ndc_ tarehe 03.03.2023, amezungumza na wananchi kupitia Vyombo vya habari kuhusu taarifa mbalimbali ikiwemo Kupatikana na Nyara za Serikali/Meno ya tembo.

Kamanda Bukumbi ameeleza kuwa Jeshi la Polisi  Mkoa wa Iringa linawashikilia watuhumiwa watatu ambao ni Henry kigulu, miaka 38, mkristo, mfanyabiashara, mkazi wa Isakalilo, Gerson Lusas, miaka 39, mfanyabiashara, mkazi wa mwangata na Elia Mkuya, miaka 55, mkulima, mkazi wa kateshi Mkoni manyara kwa kosa la kapatikana na meno ya tembo na kujihusisha na uwindaji haramu katika hifadhi ya Taifa ya Ruaha.

Hata hivyo, ACP Bukumbi ameeleza kuwa watuhumiwa hao walikamatwa katika harakati za kutaka kufanya biashara na watu waliokuwa wakiwasiliana nao, hivyo watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani baada ya upelelezezi kukamilika.

Kwa upande wake, Kamada wa Uhifadhi ya Taifa ya Ruaha Kamishna msaidizi wa Uhifadhi  Godwell Elias Ole Meing'ataki amesema kuwa mnyama tembo ni mnyama muhimu sana kwenye swala la uhifadhi lakini pia katika swala zima utalii ni moja ya kivutio kikubwa na thamani ya meno hayo ni sawa na dola za kimarekani US$ 90,000, sawa na tshs. 206,861,886/= 

Pia aliendelea kusema tukumbuke ya kwamba hii thamani ya tembo tumeitoa lakini umuhimu wa tembo katika utalii ni jambo ambalo ni kubwa sana tembo mmoja anaishi kati ya miaka sabini mpaka themanini kwaiyo tunapozungumzia tembo mmoja ameuwawa yale manufaa ambayo tungeyapata kuanzia miaka sabini mpaka themanini yanapotea kutokana na ujangili.

Halikadhalika, ACP Bukumbi alimalizia mazungumzo hayo kwa kutoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi katika kutoa taarifa kwa wakati zinazohusu viashiria vya uhalifu na wahalifu wakati wote.

Chanzo; Jeshi la Polisi.









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...