Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

Yanga SC wameendelea kushikilia msimamo wao wa kumtaka Mchezaji Feisal Salum kurejea kambini kutumikia mkataba wake hadi ifikapo mwisho wa mkataba huo, Mei 30, 2024 ikiwa ni baada kupokea maamuzi ya mrejesho wa Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji.

Taarifa ya Klabu hiyo iliyotolewa leo (Machi 6, 2023) imeeleza kuwa Klabu imemwandikia barua Mchezaji huyo kumtaka kurudi kambini haraka iwezekanavyo kuendelea kutumikia mkataba wake hadi utakapofika mwisho kama ilivyoamuliwa na Kamati hiyo ya Sheria na Hadhi za Wachezaji.

Hata hivyo, Taarifa hiyo imeeleza kuwa Yanga SC ipo tayari kumpokea Feisal na kumjumuisha kwenye Kikosi chao kwa kuzingatia sera na utaratibu wa Klabu katika kuongeza mikataba Wachezaji wake wanaofanya vizuri.

“Uongozi wa Yanga SC upo tayari kuendelea na mazungumzo na Feisal na Wawakilishi wake katika kuboresha mkataba wake endapo wataridhia kukaa chini na kufanya mazungumzo”, imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Yanga SC wamesema wapo tayari kumruhusu Mchezaji huyo kuondoka Klabuni hapo endapo atazingatia matakwa ya mkataba, na utaratibu wa sheria za uhamisho wa Wachezaji zinazotambulika na Mamlaka za Soka nchini (TFF) na duniani (FIFA). Huku wakieleza wapo tayari kufanya mazungumzo na Klabu yoyote inayomhitaji Mchezaji huyo.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...