Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha

MLEZI wa Umoja wa wanawake (UWT) Kibaha Mjini , ambae pia ni Mke wa Mbunge wa Jimbo hilo, Selina Koka amechangia kiasi cha sh.milioni Saba kwa ajili ya kutunisha akaunti za UWT kata.

Selina alitoa kauli hiyo kata ya Sofu ,katika ziara ya kamati ya utekelezaji UWT wilaya ambayo anaambatana nayo kwenye ziara ya kata 14 pamoja na kamati ndogo ndogo .

Alieleza, hadi sasa ameshatoa kiasi cha sh.500,000 kwa kata kumi na anaendelea hadi atakapomaliza ziara kwa kata zote.

"Malengo ni kuinua akaunti hizi ili kila kata iongeze nguvu katika shughuli zao ,ambapo pia kila kata ninagawa mipira na jezi kwa ajili ya michezo ya mpira wa wanawake"alifafanua Selina.

Aidha akiwa na Kamati hiyo ya utekelezaji,Selina wametoa taulo za kike kwa wanafunzi wa kike shule ya Sekondari Koka pamoja na shule ya Sekondari Tumbi.

Awali Mwenyekiti wa UWT Kibaha Mjini Elina Mgonja alieleza katika ziara hiyo wanakagua uhai wa Jumuiya na kusisitiza vikao kwenye matawi na kata.

"2024 tunaenda katika uchaguzi ,na chaguzi zote ni hesabu hivyo Lazima kujua uhai wa Chama kwa kujua idadi halisi ya wanachama wetu."alieleza Mgonja.

Mgonja amewaasa kuondoa matabaka,na kuwasisitiza wanawake kujitahidi kuisemea Serikali na viongozi waliopo madarakani juhudi za kiuchumi na maendeleo wanazozichukua .

Hata hivyo Mwenyekiti huyo alisema ,kuanzia sasa hawakai ofisini wanashuka katika ngazi za chini kuwapigania wanawake kiujasiliamali na kutoa mafunzo mbalimbali.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...