Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV -Arusha
WIZARA ya Fedha na Mipango imepongezwa na Wahariri kutoka vyombo vya habari nchini kwa namna ambavyo iko mstari wa mbele kutoa taarifa kwa wakati huku wakitumia nafasi hiyo pia kukipongeza Kitengo Cha Mawasiliano Cha Wizara hiyo kinachoongozwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kutoka Wizara ya Fedha na Mipango,Bw.Benny Mwaipaja kwa namna wanavyoshirikiana kwa karibu na kundi hilo la Wahariri na Waandishi wa Wahabari kwa Ujumla.
Wakizungumza kwenye Semina iliyoandaliwa na Wizara ya Fedha na Mipango kwa Wahariri wa Vyombo vya Habari na Wanahabari iliyoanza Jana Jijini Arusha kwa lengo la kuwajengea uelewa kuhusu Mikakati,Programu na Sera mbali mbali,Wahariri hao wametumia nafasi hiyo kuipongeza Wizara hiyo.
Mhariri wa Habari kutoka Gazeti la Nipashe Bi. Salome Kitomari amesema kwamba kitengo hicho cha mawasiliano kimekuwa kikitoa ushirikiano mkubwa katika taarifa mbalimbali ambazo zinatokea nje ya nchi licha ya changamoto ya kupishana kwa masaa baina ya nchi hizo na Tanzania lakini bado taarifa zimekuwa zikifa kwa wakati.
"Tunaipongeza Wizara na kwa kipekee tukupongeze sana Mkuu wa Kitengo na timu yake, kwa kuwa mstari wa mbele kutoa taarifa, kwa wakati hivyo kusaidia watanzania kupata fursa ya kuelewa mambo miradi mbali mbali inayotekelezwa na serikali kupitia wizara hii" alisema Bi. Kitomari
Kwa upande wake Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Kitengo cha Utangazanaji wa habari za Biashara na Uchumi Bi.Gloria Michael ameiomba Wizara hiyo kuwapeleka wahariri na wanahabari kutembelea miradi ya Maendeleo ili kupata uelewa mkubwa na mpana kuhusu miradi hiyo ya kimkakati inavyotekelezwa kupitia fedha za mikopo kutoka kwa wadau wa maendeleo.
Wakati huo huo Mwenyekiti wa Wahariri ambao wanaandika habari za Wizara ya Fedha na Mipango kutoka Azam Media Group Bw.Ben Mwang'onda ameiomba Wizara ya Fedha na Mipango kupitia kitengo cha Mawasiliano Serikalini kuendelea kufanya vizuri zaidi katika utoaji wa taarifa kwa kuwa wananchi wanapata fursa ya kutambua Majukumu na utekelezaji wa wizara hiyo ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo ya kimkakati.
"Serikali imekuwa ikitekeleza miradi ya maendeleo mikubwa pamoja na kufanya mambo makubwa lakini upatikanaji wa taarifa umekuwa wa kusua sua hali ambayo inawanyima wananchi kutambua hatua kubwa za kimaendeleo zinazopigwa na serikali” alisema Bw. Mwang’onda
Kwa upande wake Bw. Baraka Sunga ambaye ni Mhariri kutoka Savy Media Group ametoa wito kwa maofisa wengine wa taasisi za Serikali kuhakikisha kuwa wanatoa taarifa kwa wakati pindi inapohitajika.
Amefafanua kwamba licha ya Wizara hiyo kuonekana kuwa nyeti kipindi cha nyuma lakini wameweza kufanya mapinduzi makubwa na kuwafanya wanahabari kufahamu taarifa za utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa kina na kuwa sehemu ya kuelemisha jamii.
"Mmetuwezesha kutambua habari nyingi za wizara hii ambayo ni injini ya uchumi wa taifa hivyo tumekuwa tukiwalisha wananchi wetu habari za uhakika,endeleeni na mfanye iwe desturi ya wizara hata kama kuna mabadiliko basi utoaji wa taarifa usibadilike,"amesema Bw. Sunga
Semina hiyo ambayo hufanyika kila mwaka na kuwashirikisha wahariri na wanahabari kutoka vyombo mbalimbali ambao huandika habari za uchumi na fedha imelenga kuwajengea uwezo katika maeneo ya uandaaji wa Dira Mpya ya Taifa ya Maendeleo 2050, Mwelekeo wa Bajeti kuu ya serikali, Utekelezaji wa Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi (PPP) na Mafanikio ya miaka miwili ya Raisi Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Benny Mwaipaja akiwaonesha Wahariri na Waandishi wa Habari kitabu cha Mkakati wa Mawasiliano wa Wizara ya Fedha na Mipango, wakati wa Semina elekezi kwa Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini iliyoandaliwa na Wizara ya Fedha na Mipango kwa ajili ya kuwajengea uelewa wa masuala mbalimbali yanayotekelezwa na Wizara ya Fedha na Mipango, katika ofisi ndogo ya Hazina, jijini Arusha.
Mkakati huo wa Mawasiliano unatumiwa na Wizara kama mwongozo wa utekelezaji wa masuala ya Mawasiliano na kuhabarisha Umma kuhusu kazi na majukumu ya Wizara ikiwemo utekelezaji wa miradi mbali mbali ya maendeleo,aidha Bw. Mwaipaja amewaomba Wahariri hao kusoma na kuulewa Mkakati huo ili uwasaidie katika kazi zao za kila siku za kuelemisha Umma hasa katika masuala yanayohusu Fedha na Uchumi yanayotekelezwa na Wizara ya Fedha na Uchumi.
Mhariri wa Habari kutoka Gazeti la Nipashe Bi. Salome Kitomari akichangia jambo wakati wa Semina elekezi kwa wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari iliyoandaliwa na Wizara ya Fedha na Mipango kwa ajili ya kuwajengea uelewa wahariri kuhusu masuala mbalimbali yanatokelezwa na Wizara ya Fedha na Mipango, katika ofisi ndogo ya Hazina Jijini Arusha.
Mhariri wa Kituo cha Matangazo cha Radio 5 Bi.Ashura Mohamed akichangia Jambo wakati wa Semina elekezi kwa wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari iliyoandaliwa na Wizara ya Fedha na Mipango kwa ajili ya kuwajengea uelewa wahariri kuhusu masuala mbalimbali yanatokelezwa na Wizara ya Fedha na Mipango,katika ofisi ndogo ya Hazina Jijini Arusha.
Mhasibu Mkuu wa Kitengo cha Pensheni, Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Eugene Jairo akizungumza wakati akiwasilisha mada kuhusu Pensheni na Mafao baada ya kustaafu kwa wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari waliohudhuria semina elekezi ya kuwajengea uelewa wa masuala mbalimbali yanatokelezwa na Wizara ya Fedha na Mipango, katika ofisi ndogo ya Hazina, jijini Arusha.
Wahariri Mbalimbali wakifuatilia kwa umakini mada zinazotolewa kwenye semina elekezi iliyoandaliwa na Wizara ya Fedha na Mipango kuhusu masuala mbalimbali yanatokelezwa na Wizara ya Fedha na Mipango, katika ofisi ndogo ya Hazina, jijini Arusha.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Benny Mwaipaja (Katikati aliyekaa), Mwenyekiti wa Wahariri ambao wanaandika habari za Wizara ya Fedha kutoka Azam Media Group Bw. Ben Mwang'onda (Kulia aliyekaa) na Katibu wa Wahariri ambao wanaandika habari za Wizara ya Fedha kutoka Clouds Media Group Bi. Joyce Shebe wakiwa katika picha ya Pamoja na wahariri mbalimbali baada ya ufunguzio wa semina elekezi kwa wahariri hao iliyoandaliwa na Waziri wa Fedha na Mipango kuhusu masuala mbalimbali yanatokelezwa na Wizara ya Fedha na Mipango, katika ofisi ndogo ya Hazina, jijini Arusha.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...