Njombe


Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt,Samia Suluhu Hassan imeidhinisha Shilingi Bil.15.4 kwa ajili ya kuwalipa fidia wananchi ili kupisha mradi wa kimkakati wa makaa ya mawe wa Mchuchuma na Liganga uliopo katika wilaya ya Ludewa mkoani Njombe,ambao unatarajiwa kuanza mara moja, baada ya serikali kukamilisha makubaliano na wawekezaji.

Afisa mwandamizi kitengo cha mipango kutoka shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Florian Mlamba, ameweka bayana wakati akizungumza na wananchi wa wilaya ya Ludewa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Mundindi.

“Tunaomba ushirikiano wenu kwenye mambo ya msingi ikiwemo kila mmoja kuwa na akaunti,kwa kadri tutakavyo maliza mapema ndivyo fedha za malipo zitaingizwa kwenye akaunti zenu mapema na matarajio yetu mwezi huu mwishoni tuwe tumeishaziingiza.” Amesema Mlamba.

Mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga amewaomba wananchi kutumia fedha watakazozipata kwa ajili ya uwekezaji kwa kuwa wamekuwa wakisubiri kwa muda mrefu.

“Fedha hizo zikiingia,zitumieni vizuri zisiwachanganye,fanyeni uwekezaji lakini pia mnavyohama, basi zingatieni na athari za kimazingira,”amesema Kamonga.



 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...