MFALME Charles III amekula kiapo kwenye hafla maalum ya kumtawaza kuwa mfalme leo Mei 06, 2023, na kwamba ameahidi kuongoza kwa kufuata sheria na kulinda amri za Mungu, uhuru kwa watu wa imani zote, kulinda raia na kuwa mtumishi wa Muungano wa Britania unaojumuisha Uingereza, Wales na Scotland, pamoja na Ireland ya Kaskazini.

Akiwa mtoto wa kwanza wa Malkia Elizabeth II, Mfalme Charles lll ametawazwa na mke wake Camilla 'Queen Consort.' Mfalme Charles III amevikwa taji kichwani saa sita adhuhuri saa za London, anakuwa mfalme wa 40 tangu kutawazwa kwa Mfalme William I mwaka 1066.

Mfalme Charles III na mkewe Camilla wamesafiri kwenye Gari Maalum katika Msafara wa Mfalme kwa umbali wa kilomita mbili kutoka Kasri la Buckingham hadi Westminster Abbey katikati mwa jiji la London.

Hafla hiyo imekuwa adhimu kwa na pekee kwa Uingereza kwa kipindi cha miaka 70, pia ni ya pili katika historia kwa kurushwa katika runinga.

Watu maarufu wapatao 2,200 akiwemo Waziri mkuu wa Uingereza Rish Sunak, mke wa Rais wa Marekani Bi. Jill Biden na mwanamuziki Katty Perry wamehudhuria hafla hiyo ukilinganisha na watu 8000 waliohudhuria hafla ya kutawazwa Malkia Elizabeth II mwaka 1953.

Mfalme Charles lll alirithi ufalme mnamo Septemba 8, 2022 kufuatia kifo cha Mama yake Elizabeth II ambaye alikuwa Malkia tangu Februari 6, 1952 alipomrithi Mfalme George VI. Wakati huo Mfalme Charles lll Charles alikuwa na umri wa miaka mitatu.

 


KSOMA ZAIDI TAARIFA MBALIMBALI KUHUSU TUKIO HILO HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...