Norwegian Church Aid  Tanzania pamoja na washirika wamezindua msafara wa vijana, kisiwani Pemba kuhamasisha Amani na Utengemano  wa jamii, wenye ujumbe ‘’ Amani Yetu, Kesho Yangu’’. Msafara huo utapita katika Wilaya nne ikiwemo Chake Chake, Mkoani, Wete na Micheweni ( Nizar Seleman Utanga (Afisa Uchechemuza na Mawasiliano - NCA-Tanzania (Picha 1)

Msafara wa vijana wenye ujumbe "Amani Yetu, Kesho Yangu’’ unawaleta pamoja mabalozi wa amani, vijana, wanaume, wanawake,   viongozi wa dini mbalimbali pamoja na wawakilishi toka asasi za kiraia   (2)

Msafara huo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa Amani na Utengamano wa jamii unaotekelezwa Zanzibar na Pemba tangu mwaka 2020. Mradi huo unatekelezwa na Norwegian Church Aid kwa kushirikiana na Zanzibar Interfaith Centre/Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dayosisi ya Mashariki na Pwani (KKKT DMP) na Ofisi ya Mufti Zanzibar kwa ufadhili kutoka Ubalozi wa Norway nchini Tanzania.   ( 3 )

Kupitia mpango huu, mafunzo mbalimbali yamewezeshwa yakiwalenga vijana, wanawake, wasichana na viongozi wa dini ili kuimarisha uwezo wao katika kujenga amani na kuimarisha mahusiano ya dini mbalimbali. Aidha,  nyenzo mbalimbali zimeendelea kutumika ikiwemo utenzi, michezo,  maigizo na ngonjera ili kuongeza vionjo na kufikisha ujumbe kwa jamii.   (4)

Timu za Amani za wilaya ya Wete na Micheweni zikichuana kuwania kombe la Interfaith Amani 2023 lililoandawaliwa na shirika la Makanisa Norway kwa ufadhili wa Ubalozi wa Norway Tanzania (5)










Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...