*Asema akitangaza mshahara na bei ya bidhaa nazo zitapanda, hivyo hatangazi hadharan

*Awapongeza TUCTA kuwa wapole mwaka huu,agusia usalama pahala pa kazi


Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV -Morogoro

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewahakikishia wafanyakazi wa sekta ya umma kwamba maslahi yao ikiwemo mishahara itaboreshwa kimya kimya kuepuka bei za bidhaa kupanda

Akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi leo Mei Mosi ,2023 Mjini Morogoro ambako Maadhimisho hayo yamefanyika Kitaifa na kuhudhuriwa na viongozi wa ngazi mbalimbali pamoja na wafanyakazi wa sekta mbalimbali,Rais Samia amesema mwaka huu suala la kuboresha maslahi na mishahara hatatangaza bali ni mwendo wa kimya kimya.

"Mwaka huu kuhusu mishahara na maslahi ya Wafanyakazi hatutatangaza hapa, tutaboresha kimya kimya maana ukitangaza hapa na wenzetu huko nao wanapandisha bei ha bidhaa na kufanya kuwepo na mfumuko wa bei, hivyo niwahakikishie wafanyakazi tunakwenda kuboresha.

"Na bahati nzuri mwaka huu TUCTA wamekuwa wa pole, hawakuwa na maneno mengi yenye moto mkali, lakini kwa kazi ambayo Serikali tumefanya kwa wafanyakazi wa sekta ya umma hata TUCTA wameridhika lakini ni wahakikishe tunakwenda kuboresha maslahi,"amesema Rais Samia.

Kuhusu makato ya kodi ,Rais Samia amesema watakwenda kukaa na kuangalia kwenye maeneo ambayo lazima yakatwe Kodi basi itakatwa na kwenye maeneo ambayo hayana ulazima basi hawataka kodi." Kulikuwa na kilio cha makato ya kodi.

"Nimeshuhudia mtu anaondoka na Sh.milioni 12 hapa, kwanini asikatwe kodi.Kodi ambayo inakatwa ndio kesho inarudi tena huku huku. Kwenye maeneo ambayo yana ulazima yatakatwa Kodi, na Yale ambayo hayana ulazima wataangalia namna ya kuondoa,"amessema Rais Samia.

Akizungumzia waajiri kutopeleka makato ya wafanyakazi wao na kusababisha kuwepo kwa malalamiko na kilio cha madai, Rais Samia amemuagiza Waziri kwenda kuitisha kikao na waajiri ili kuondoa kuzungumza nao na kisha kumalizia kilio cha waajiri kutopeleka makato.

Kuhusu Madai ya bima ya afya kwa wafanyakazi ametoa maelekezo ya kwamba madai yalipwe ndani ya Siku 60 ili wafanyakazi wapate haki yao ya matibabu huku akitumia nafasi hiyo kuzungumzia hatua ambazo zimekuwa zikichukuliwa na Serikali katika kufuata mikataba ya Kimataifa inayozungumzia afya na usalama pahala pa kazi

"Serikali kupitia OSHA tumekuwa tukihakikisha afya na usalama pahala pa kazi na katika kuhamasisha OSHA wanatekeleza majukumu yao tayari tumeongeza wafanyakazi 18 na tumenunua magari 13 ili kazi ifanyike vizuri.

"Wakati mwakilishi wa ILO nchini Tanzania anazungumza ameeleza kuhusu mikataba ya Kimataifa kuhusu usalama mahala pakazi. Tanzania tunaelewa vema na nchi yetu imeanza kufanyia kazi muda mrefu kuhusu suala la afya na usalama kazini.Tunayo na sheria ya usalama na afya mahala pakazi.

"Pia pamoja na mambo mengine kumeundwa Baraza la kusikiliza changamoto na yote hiyo ni kuendana na mikataba ya Kimataifa kuhusu afya na usalama mahala pakazi,nchi yetu ilishaona umuhimu wa kumlinda mfanyakazi, amessema Rais Samia alipokuwa akitoa hotuba yake mbele ya Wafanyakazi na Watanzania kwa ujumla sambamba na kujibu baadhi ya hoja ambazo zimetolewa wakati wa Maadhimisho hayo.

Kuhusu malalamiko ya Madai ya malimbilikizo kwa watumishi was Hospitali teule, Rais Samia amesema ni kuna madai lakini kinachoendelea kwa sasa ni kupitia madai hayo kwa kufanya ukaguzi ili kuhakikisha wote wanaostahili kulipwa , wanalipwa.

"Tuliposema tunalipa malimbilikizo hayo ilikuwa ni kuwalipa madaktari na Watoa huduma za matibabu lakini tulipoanza kufanya uhakiki tukakuta wanaodai wapo mpaka na madereva, lakini niwahakikishie baada ya kufanya upembuzi wote wanaostahili watalipwa."









 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...