Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla amewakumbusha waumini wa dini ya kiislam na wananchi wote kuwa miongoni mwa neema kubwa kwa mwanaadamu ni kuwa na wazazi wawili ambao tunapaswa kuwatendea wema wakiwa hai na kuwakumbuka kwa duwa watakapotangulia mbele ya haki.
Akiwasalimu waumini wa Masjid Tawbah Kisauni katika Ibada ya Sala ya Ijumaa, Alhajj Hemed amesema kuwafanyia wema wazazi wawili ni miongoni mwa ibada kubwa ambayo hujenga mahusiano mazuri baina ya wazazi na watoto wake na kuongeza mapenzi katika Familia.
Sambamba na hayo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameeleza kuwa Uislamu umehimiza suala la maendeleo hivyo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inayoongozwa na Rais Alhajj Dkt. Hussein Ali Mwinyi imedhamiria kurahisisha upatikanaji wa huduma za Elimu, Afya na uimarishaju wa Miundombinu ya Barabara na Mawasiliano.
Aidha amewataka wananchi kuunga Mkono jitihada zinazochukuliwa na Serikali yao kwani dhamira yake ni njema ikiwa ni pamoja na kusimamia maslahi yao na kuwawekea mazingira bora kiuchumi na kijamii.
Akitoa Khutba ya Sala ya Ijumaa Shekh Masoud Mtumwa Khamis amewataka wazazi na walezi kusimamia malezi ya watoto wao na kukemea tabia ya baadhi ya wazazi kuwatelekeza watoto hatua ambayo inapelekea watoto hao kukosa malezi ya karibu ya wazazi wao.
Aidha ameeleza kuwa ni wajibu wa waumini wa Dini ya Kiislamu na wananchi kwa ujumla kuunga Mkono juhudi za Serikali hasa katika kupinga matendo ya udhalilishaji, rushwa na matumizi ya madawa ya kulevya vitendo ambavyo vinachangia kupotea kwa nguvu kazi ya Taifa letu.
Home
JAMII
MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR AWAKUMBUSHA WAUMINI DINI YA KIISLAMU NA WANANCHI KUWATENDEA WEMA WAZAZI WAO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...