Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imetangaza kukamilika kwa tarataibu ambazo zimewezesha Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kupata mkopo wa Dola za Kimarekani milioni 200 sawa na shilingi za Kitanzania bilioni 470.

NBC benki ni mwezeshaji mkuu ikishirikiana na benki ya NMB kama mkopeshaji mwenza katika kufanikisha upatikanaji wa mkopo huu mkubwa kwa Zanzibar.

Fedha zinazotokana na mkopo huo zitasaidia kutekeleza miradi mbali mbali ya kijamii pamoja na miundo mbinu malengo yakiwa ni kuboresha maisha na hali ya kiuchumi kwa Wazanzibari.

Huu ni ushirikianao wa aina yake ambapo Benki ya NBC imeweza kufanya kazi na SMZ katika jitihada za kufanikisha miradi ya maendeleo kwa ustawi wa wananchi wa Zanzibar.

Mkurugenzi Mtendaji wa NBC Theobald Sabi, alisema benki ya NBC inafurahi kuweza kusaidia upatikanaji wa mkopo huo utakaosaidia SMZ kufikia malengo yake ya ukuaji wa uchumi na maendeleo jumuishi.

Sabi alisema mkopo huo ni hatua kubwa na muhimu katika kushirikiana pamoja kwenye malengo ya maendeleo endelevu na kuboesha maisha ya wananchi wa kisiwa cha Zanzibar. Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa benki ya NBC itaendelea kuwa mstari wa mbele katika kusaidia jitihada za kuleta maendeleo ya kiuchumi kupitia huduma za kifedha.

Kwa upande wake, Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ally Mwinyi alishukuru benki ya NBC kwa kuweza kufanikisha mkopo huo ambao alisema utakuwa na mchango mkubwa katika kufadhili miradi ya maendeleo Zanzibar na hivyo kukifanya kisiwa hicho kufikia malengo yake ya kuboresha maisha ya wananchi wake kwenye njanja za kijamii na kiuchumi.

Dkt. Mwinyi alitaja baadhi ya maeneo ambayo yatanufaika na fedha hizo kuwa ni huduma za kiafya, elimu, miundo mbinu ya usafiri, na miradi ya maendeleo ya kijamii.

“Kwa kuwekeza kwenye sekta hizi muhimu SMZ inalenga kuboresha maisha ya wananchi wake na kuongeza wigo wa upatikanaji wa huduma muhimu za kijamii na kuwezesha kufikia malengo ya muda mrefu ya maendeleo ya kiuchumi,” alifafanua 

Rais wa Zanzibar Dkt. Ally Mwinyi  (katikati) akishududia Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Theobald Sabi  (kushoto) na Katibu Mkuu Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Zanzibar Dkt. Juma Malik Akili wakisaini mkataba utakowezesha Zanzibar kupata mkopo wenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 200 sawa na shilingi bilioni 470 kwa ajili ya kusaidia maendeleo ya Zanzibar. Mkopo huo umetolewa na benki ya NBC ikiwa kama mwezeshaji mkuu kwa kushirikiana na benki ya NMB.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...