Na Mwandishi Wetu

MKUU  wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mdeme amewataka wafanyabiashara ndogondogo maarufu Machinga kujiunga na mfumo wa Kanzi  data ambao utarahisisha kutatua matatizo ya kiuchumi na kijamii ikiwa ni pamoja na kurahisisha mfumo wa bima ya afya .

Akizungumza wakati akihitimisha kongamano la Shirikisho la Umoja wa Wamachinga (Shiuma) lililoambatana na uzinduzi wa Kanzi data kwa jailli ya machinga na wajasiliamali nchi nzima kupitia vocha maalumu lililofanyika wilayani Kahama mkoani Shinyanga Mdeme amesema zoezi hilo litawaweka wamachinga pamoja.

"Kanzi data itasaidia kujua idadi kamili ya wamachinga hadi wanapokaa maeneo ambayo hayafikiki na hivyo kurahisha utatuzi wa maswala mbali mbali yakiwemo ya afya pia Shiuma itaweza kuwatambua kwa usahihi ,idadi na mahali walipo wanachama wake.

Kwa upande wake  Mkurugenzi wa TIVA Tanzania James Mhingo anasema kumekuwa na pengo la kiteknojia  hali iliyopelekea kukosekana kwa mifumo dhabiti na ya kisasa inayoweza kuunganisha kidigitali hospitali zote nchini na watoa huduma wakiwemo walengwa ambayo ni jamii kwa ujumla hivyo wameamua kuanza kutengeneza mfumo kwanza kabla ya bima yenyewe.

"Tumeanza na uzinduzi wa mfumo  kanzi  data kwa makundi maalumu wakiwemo  machinga /wajasiliamali hii itawezesha  kujua idadi yao Kila mkoa na nchi nzima  na pia  kuwezesha kupatiwa huduma za Bima ya Afya hapo badae mfumo utakapokamilika”, Amesema Mhingo na kuongeza

"Jamii imekuwa ikitumia mifumo duni na isiyoendana na wakati katika kuwafikia wateja hivyo watakapo kuwa kwenye mfumo itawarahisishia kupatiwa huduma mbali mbali”

Mhingo amesema Kampuni ya TIVA itatumia mfumo wake wa teknologia ambayo inatumia vocha ambazo zitapatikana kote nchini  na pia watu watajisajili kwa kutumia  simu katika kusajili wanachama hivyo tumeanza na wanachama wa Shiuma  lengo kubwa ni kuwarahishia kujisajili kwa kutumia  bima mkononi kwa Kila mtu atakayehitaji nchi nzima.

Aidha Mwenyekiti wa wamachinga Mr Mboto amesema kuwa kutokana na mfumo huo utawasaidia kuondoa changamoto za kuweza kuwatambua kwa usahihi ,idadi na mahali waliko wanachama wake pia itatumika kwa matumizi mengine ya kiofisi na kiutawala.

"Kanzidata hii itasaidia katika kuandaa na kuratibu shughuli zote za utoaji huduma ya bima ya afya  itakapoanza pia itasaidia kimawasiliano na katika kutatua changamoto mbalimbali” amesema Mboto

Pamoja na hayo Mkurugenzi wa Fedha na Masoko Tiva Tanzania , Mark Irunde amesema takwimu zinaonyesha  asilimia 15 tu ya  Watanzania wanabima za afya na hivyo kuacha  asilimia 85 ambao hawana na hivyo kutegemea zaidi fedha ambazo mgonjwa atakuwa nazo wakati anaumwa.

Amesema hali hii hupelekea kutegemea msaada kutoka kwa ndugu ,marafiki katika kugharamia matibabu ya mgonjwa na hii huwaweka watu wengi katika hatari ya kupoteza maisha hivyo kupitia zoezi hili la kanzi data itarahisha wananchi kupata matibabu kwa njia rahisi kupitia mfumo wa bima .

Tiva ambayo ni Kampuni mpya ya Bima inatarajia kusajili Watu milioni 3.8(watu milioni tatu na laki nane) na kwamba  asilimia 8 ya watanzania watajisajil kupitia simu za mkononi.

“Bima hii ni soko huria, kwa utumiaji wa Kanzi data mteja ataweza kuona  invoice  mgonjwa akiwa hospital kupitia kwenye mfumo, na hakutakuwa na  kufoji.

"Tunawafungia mfumo huu wa kanzidata katika  hospitali  bure nchi nzima kwenye hospitali zote,  na mfumo huu utaonana na mifumo mingine."



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...