Na. Damian Kunambi, Njombe.

Wakazi wa kata ya Lugarawa wilayani Ludewa mkoani Njombe wameaswa  kujenga nyumba kwaajili ya kupangisha wanafunzi watakaoanza masomo katika chuo cha ufundi stadi (VETA) kinacho tarajiwa kuanza kudahili wanafunzi mapema mwaka ujao.

Hayo ameyasema mbunge wa Jimbo la Ludewa Joseph Kamonga alipofanya mikutano katika vijiji vya Shaurimoyo, Mdilidili pamoja na Lugarawa ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kutembelea vijiji vyote vya jimbo hilo kwa lengo la kutoa mrejesho na kusikiliza changamoto ambapo mpaka sasa tayari amekwisha tembelea vijiji 30 kati ya 77 vya jimbo hilo.

 Chuo hicho cha ngazi ya mkoa kinacho gharimu kiasi cha sh. Bil. 5.4 kinaendelea na ujenzi wake katika kijiji cha Shaurimoyo katani humo kwa sasa kimefikia asilimia 93 ya ujenzi na kinatarajiwa kupokea wanafunzi wasiopungua 1000 wa fani mbalimbali huku mabweni yaliyopo chuoni hapo yakitosheleza wanafunzi 350 pekee.

" Ndugu zangu kuanzishwa kwa chuo hiki ni fursa ya kipekee kwenu hivyo naomba muitumie, ukiangalia idadi ya wanafunzi watakaoishi bwenini ni wachache hivyo kuna wanafunzi 650 watakosa makazi, kwahiyo hii ni fursa kwenu ya kujenga nyumba za kupangisha hao wanafunzi".

Sanjali na ujenzi huo wa nyumba za kupangisha lakini pia amewaasa kuanzisha biashara mbalimbali ikiwemo za vyakula ili kuweza kujiongezea kipato na kukuza uchumi wa kata na wilaya kwa ujumla.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...