Na Mwandishi wetu - Dodoma.

Serikali imetoa rai kwa wazalishaji wa bidhaa zote za viwandani kuongeza jitihada za uzalishaji wa bidhaa kwa ubora unaohitajika sokoni na kwa kufuata Sheria, Kanuni na Taratibu zilizowekwa ili kukabiliana na kupanda kwa bei za bidhaa mbalimbali nchini.

Waziri wa viwanda na biashara Dkt Ashatu  Kijaji ameyasema hayo Julai 25, 2023 alipokuwa akitoa Taarifa ya tathimini ya Mwenendo wa Bei za Bidhaa Muhimu Nchini  2022/2023 na 07/ 2023 katika Mkutano wa Waandishi wa Habari uliofanyika Mtumba, Dodoma.

Aidha, amewatahadharisha wazalishaji, wasambazaji au wanunuzi wa bidhaa yoyote ile kutokuongeza kiholela bei ya bidhaa  bila sababu ya msingi na  kuwataka Maafisa Biashara katika Halmashauri zote Nchini kusimamia ipasavyo bei za bidhaa ili kuwalinda wazalishaji na walaji.


Vilevile, Waziri Kijaji amesema mwenendo wa bei za bidhaa muhimu kwa Julai 2023 imeonesha bei ya mazao ya mahindi, unga wa mahindi, mchele, maharage, viazi mviringo na unga wa ngano imeshuka, bei ya sukari na mafuta ya kupikia ni himilivu, wakati bei ya vifaa vya ujenzi kama saruji imeongezeka kidogo wakati bei ya nondo na bati ni himilivu.


Aidha, Waziri Kijaji amebainisha kuwa uzalishaji wa sukari nchini kwa mwaka 2023/24 umeimarika kwa kuwa Tanzania ina jumla ya viwanda vikubwa vitano (5) vya kuzalisha sukari vikiwemo TPC, Kagera Kilombero, Mtibwa na Bagamoyo ambavyo vina uwezo wa kuzalisha tani 75,000 kwa mwezi wakati mahitaji ni tani 38,000 na hivyo kubaki na ziada ya tani 37,000.

 Akifafanua zaidi kuhusu uzalishaji wa saruji nchini, Dkt. Kijaji amesema Tanzania ina viwanda 14 vyenye uwezo wa kuzalisha tani 10,850,000 za saruji kwa mwaka  ambapo mahitaji ya ndani ya nchi ni tani 7,100,000 na kubakiwa na ziada ya tani 3750,000 inayouzwa nje ya nchi hususani nchi za Congo, Rwanda, Uganda, Malawi, Zambia na Msumbiji.


Kwa upande wa bidhaa za chuma, Amesema Tanzania ina viwanda 25 vinavyozalisha chuma na bidhaa za chuma kama nondo, mabomba, misumari na seng’enge ambapo Viwanda 16 vinauwezo wa kuzalisha nondo tani 750,000 kwa mwaka ambapo mahitaji nchini ni tani 550,336 na ziada ya tani 199,664 huuzwa nje ya nchi.


WAziri wa viwanda na biashara Dkt Ashatu Kijaji akizungumzia na wanahabari ( hawapo pichani) wakati akitoa taarifa ya tathimini ya mwenendo wa bei za bidhaa muhimu Nchini 2022/2023 na julai 2023, Mtumba Dodoma

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...