RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amemuagiza Mkurugenzi mwendeshaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) kuwasilisha kwake orodha ya majina ya waajiri wasiowasilisha michango ya waajiiriwa wao kwenye Mfuko huo ili awachukulie hatua kwaajili ya kulinda haki za watu.
Dk. Mwinyi alitoa agizo hilo ukumbi wa hotel ya Golden Tulip, uwanja wa ndege, Mkoa wa Mjini Magharibi kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 25 tangu kuanzishwa kwa ZSSF.
Alisema, kazi kubwa inayoendelea kufanywa na ZSSF ni mabadiliko na huduma bora kwenye sekta ya uwekezaji wa miradi mbali mbali ya maendeleo inayogusa jamii moja kwa moja.
“Miradi yote inayotekelezwa na iliyopangwa kutekelezwa na ZSSF sina shaka itaongeza faida kwa ZSSF, itakuza uchumi na kutoa fursa nyingi za ajira nchini” Alisifu Rais Dk. Mwinyi.
Alisema, ZSSF inatokana na ushirikiano baina ya Serikali, Waajiri na Waajiriwa, hivyo alizitaka taasisi za Serikali na Jumuiya zote kuwasilisha michango yao kwa wakati ili kurahisisha shughuli za uendeshaji wa taasisi hiyo kwa lengo la kuwajengea misingi mizuri wafanyakazi wao wanapostaafu au wanapohitaji mafao yao.
Pia Rais Dk. Mwinyi alizitaka Taasisi za Serikali zishirikiane kutoa huduma ili kuwaondolea usumbufu usio wa lazima wananchi.
Kadhalika, aliwaomba wajasiriliamali wajisajili ili wachangia kwenye Mfuko wa hiari kwani una faida hasa pale biashara zao zitakapotetereka au watakapohitaji mafao ya aina yoyote.
Akitoa ushuhuda kwa mataifa yaliyoendelea duniani, Rais Dk. Mwinyi alieleza lengo la kuanzishwa kwa sekta za huduma za jamii ni kukusanya michango, kuwekeza na kulipa mafao kwa mujibu wa sheria zilizopo.
Aidha, alieleza Sekta hiyo pia hutumika kuinua uchumi wa nchi na wananchi hasa kwenye uwekezaji wa miradi mikubwa yenye tija.
Alisistiza, Sekta ya hifadhi ya jamii ni nguzo muhimu ya uchumi inayotegemewa na nchi pamoja na wafanyakazi.
Alieleza licha ya mafanikio makubwa ya ZSSF ndani ya miaka 25 tokea kuanzishwa kwake, lakini bado haijawekeza kwenye miradi mikubwa zaidi, hivyo, aliieleza taasisi hiyo ina wajibu wa kujifunza kwa wengine ili kuongeza ufanisi kwenye uwekezaji wenye tija zaidi.
Pia, aliipongeza ZSSF kwa utekelezaji wa agizo lake la kuongeza pensheni kwa wastaafu wa kima cha chini kutoka shilingi 90,000 hadi 180,000 kama Serikali ilivyoongeza kwa wastaafu wanaolipwa kupitia Wizara ya Fedha.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango, Dk. Saada Mkuya Salum, alieleza malifakutoa mafao kwa wastaafu lakini pia ZSSF imegusa hudua zote za jamii zikiwemo, Afya michezo, elimu vituo vya daladala na huduma nyengine kwa wananchi.
Naye, Mkurugenzi Mwendeshaji Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar, Nassor Shaaban, alieleza lengo la kuunzishwa kwa Mfuko huo ni kutoa ulinzi na kinga kwa wanachama wake kwa kutoa pencheni na mafao mbalimbali.
Akizungujmzia mafanikio ya ZSSF kwa kipindi cha miaka miwili ya Dk Mwinyi alieleza ni pamoja na utekelezaji wa Ilani ya CCM ya 2025 nakuonengeza hadi sasa Mfuko umetekeleza miradi ya maendeleo kwa asilimia 90, pamoja na kutekeleza jukumu la kisheria la mfuko ikiwemo kusajili mwanachama, uwekezaji pamoja na ulipaji wa mafao na pencheni.
Miongozi mwa mafao yanayotolewa na ZSSF ni pamoja fao la kustaafu, uzazi, fao la wenye ulemavu, kuumia kazini na fao la wajasiriamali. ZSSF ilianzishwa rasmi mwaka 1998, maadhimisho ya miaka 25 ya taasisi hiyo yalikwenda sambamba na kauli mbiu, “Nidhamu, Uwajibikaji teknolojia ya sasa na uwekezaji endelevu na mafao bora kwa wanachama”.
IDARA YA MAWASILIANO, IKULU ZANZIBAR
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi TUZO Mchangiaji Bora wa ZSSF Mfuko wa Hiyari ZVSSS Ndg. Said Kapela (kulia kwake) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar Mhe.Dkt. Saada Mkuya Salum na (kushoto kwa Rais ) Mkurugenzi Muendeshaji Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) Nassor Ameir, wakati wa hafla ya Maadhimisho ya Miaka 25 ya ZSSF iliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Mjini Unguja leo 25-7-2023 Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa TUZO Maalumu na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar Mhe.Dkt. Saada Mkuya Salum, wakati wa hafla ya Maadhimisho ya Miaka 25 ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) iliyofanyika katika ukumbi wa HGoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja leo 25-7-2023, na (kushoto kwa Rais) Mkurugenzi Muendeshaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) Ndg. Nassor Ameir.(Picha na Ikulu)RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizindua Mfumo wa ZSSF WHATSAPP na Uzinduzi wa Nyumba za Mji wa Dk. Hussein Mwinyi –Mombasa Zanzibar wakati wa Maadhimisho ya Miaka 25 ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) na (kulia kushoto kwa Rais)Mkurugenzi Muendeshaji wa ZSSF.Ndg. Nassor Ameir, hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja leo 25-7-2023 Jijini Zanzibar na (kulia kwa Rais) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar Mhe.Dkt.Saada Mkuya Salum.(Picha na Ikulu)WAKUU wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama Zanzibar wakifuatilia hutiba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akihutubia katika hafla ya Maadhimisho ya Miaka 25 ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) iliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja Jijini Zanzibar leo 25-7-2023.(Picha na Ikulu)RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihutubia katika hafla ya Maadhimisho ya Miaka 25 ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) iliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja leo 25-7-2023 Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)MKURUGENZI Muendeshaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF)Ndg. Nassor Ameir akizungumza na kuelezea mafanikio ya ZSSF kwa kupindi cha miaka 25 ya mfuko huo, wakati wa hafla ya Maadhimisho ya Miaka 25 ya (ZSSF) iliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja Jijini Zanzibar leo 25-7-2023.(Picha na Ikulu)WAGENI waalikwa katika hafla ya Maadhimisho ya Miaka 25 ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akihutubia katika maadhimisho hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja Jijini Zanzibar leo 25-7-2023.(Picha na Ikulu)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...