Njombe
Wananchi wa kijiji cha Makanjaula kata ya Uwemba halmashauri ya mji wa Njombe hatimaye wameanza kuona mwanga wa umeme tangu Dunia ilipoumbwa mara baada shirika la umeme Tanzania (TANESCO) mkoa wa Njombe kufanikiwa kuwasha umeme katika kijiji hicho.
Diwani wa kata ya Uwemba Jactan Mtewele ametoa shukrani kwa shirika hilo kutoa ushirikiano wa kutosha mpaka ilipofikia hatua ya uwashaji wa umeme kwa kwa kuwa wananchi wa kijiji hicho walikuwa wakitegemea umeme wa sola pamoja na uliotengenezwa na mtu binafsi.
"Tokea tunapata uhuru kijiji hiki hakijawahi kuwa na umeme kwa hiyo ninamshukuru sana Mungu kwa kuingia kwenye historia nikiwa kama diwani wa kata hii kwa kijiji hiki kupata umeme na vile vile tunawashukuru sana ndugu zetu wa TANESCO kwa kutupa ushirikiano mpaka leo tunafikia hatima ya uwashaji wa umeme"alisema Mtewele
Mara baada ya zoezi la uwashaji wa umeme Afisa mahusiano kutoka shirika la umeme Tanzania TANESCO mkoa wa Njombe Neema Lyakulya na wataalmu wengine wametoa elimu juu ya matumizi bora ya nishati bila kuleta madhara ambapo pia wametoa wito kwa wananchi kutunza miundombinu ili kuepusha uharibifu pamoja na ukatikaji wa umeme.
Siglada Mwalongo na Alto Manga ni miongoni mwa wakazi wa kijiji hicho wameshukuru serikali kwa kuwafikishia nishati kwa kuwa itasaidia kukuza maendeleo ya kijiji huku pia wakiomba TANESCO kuwafikishia nishati hiyo maeneo yote ya kijiji.
"Huduma nyingi za msingi tulikuwa tunazikosa kutokana na kutokuwepo kwa nishati,watoto walikuwa wanasoma kwa kutumia solar kwa hiyo jua lisipowaka watoto hawawezi kusoma lakini pia mitihani ya wtoto tulikuwa tunakwenda kudulufua umbali mrefu kule Uwemba na kwa ghalam kubwa lakini pia tulikuwa tunenda kusaga mbali ila kwasasa tutakuwa tunasaga hapa hapa"amesema Siglada Mwalongo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...