Na Andrew Chale, Dar es Salaam.
JUMUIYA ya Watanzania waliowahi kusoma Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Marekani- Afrika (The USIU-A Tanzania Alumni Chapter) kilichopo Jijini Nairobi, Kenya wameadhimisha miaka 4 tangu kuzaliwa kwa Jumuiya hiyo siku ya Jumamosi julai, 2023 Dar es Salaam.
Akizungumza katika tukio hilo lililoenda sambamba na chakula maalum cha jioni kwa wanachama wake, Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo kwa upande wa Tanzania, Glen Kapya ameeleza kwamba Makao Makuu ya Jumuiya hiyo yapo Nairobi, Kenya na Wanachama wanatoka Nchi mbalimbali ndani na nje ya Bara la Afrika.
"Chombo hiki kinakutanisha wadau hawa kustawisha maendeleo ya Chuo hicho na wao binafsi sambamba na kupeana fursa mbalimbali, kudumisha udugu, umoja na ushirikiano ambao umekuwepo miaka mingi." Amesema Glen Kapya.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Jumuiya hiyo USIU-A, Bw. Kris Senanu amepongeza Wana Jumuiya ya Tanzania kwa jukumuika pamoja kwani ni utaratibu mzuri katika maisha ya Wanadamu na kitaaluma.
"Wanafunzi kutoka mataifa zaidi ya 23, wamepita katika chuo hiki, tuendelee kujipongeza na kukuza umoja wetu, nawashukuru sana Tanzania ni nchi nzuri na ni Mabalozi wazuri wa wa ASIU-AFRIKA " amesema.
Jumuiya hiyo ina zaidi ya Wanachama 200 , huku ikikadiriwa wanafunzi zaidi ya 500 tokea kuanzishwa kwake kutoka Tanzania na nchi zingine za Afrika na nje ya Afrika.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...