Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana Julai 17, 2023 amewasili wilayani Ludewa kwa ajili ya Ufunguzi wa Kuambiana Cup utakaofanyika Julai 18, 2023 katika Uwanja wa Ngelenge Manda wilayani hapo.

Mhe. Pindi Chana alipata nafasi ya kuzungumza na uongozi wa Wilaya ya Ludewa ukiongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo, Mhe. Victoria Mwanziva ambapo ameipongeza wilaya hiyo kwa kutekeleza na kusimamia miradi ya maendeleo wilayani hapo pamoja na kutenga eneo la uwanja wa michezo ambapo amewaahidi kutuma wataalam kutoka wizarani kuona eneo hilo na kutoa ushauri wa kitaalam kuhusu ujenzi wa Viwanja vya Michezo.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya hiyo, Mhe. Victoria amempongeza Mhe. Waziri Balozi Dkt. Chana kwa namna anavyofuatilia maendeleo ya wilaya hiyo pamoja na kuunga mkono shughuli za maendeleo ikiwemo kugawa vifaa vya michezo katika shule, mabati ya ujenzi wa bweni la Shule ya Madilu na kuunga mkono wajasiriamali wa wilaya hiyo.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...