Mkurugenzi Mtendaji wa Bank of Africa Tanzania,Adam Mihayo akiongea wakati wa kongamano hilo.
Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo na wakati, Bi. Ninael Mndeme akitoa mada.
Mkurugenzi Mtendaji,Adam Mihayo na maofisa wengine wa Bank of Africa Tanzania wakifuatilia mada.
Baadhi ya wafanyabiashara walioudhuria wakifuatilia mada za wataalamu mbalimbali.
Picha ya pamoja ya Wafanyakazi wa Bank of Africa kutoka vitengo mbalimbali waliohudhuria katika kongamano hilo.

BANK of Africa Tanzania mwishoni mwa wiki imekutana na wajasiriamali , katika warsha iliyoandaliwa na benki hiyo ikiwa na kauli mbiu ya “TUKUE PAMOJA”, kwa dhumuni kubwa la kutoa elimu ya kina ya kifedha, namna bora ya kuhifadhi kumbukumbu za kibiashara, majadiliano ya kina kuhusu mada mbalimbali za kodi, na mikakati ya kuongeza uwezo wa huduma za benki ili kuchochea ukuaji wa mitaji.

Akifungua warsha hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Bank of Africa Tanzani, Bwana. Adam Mihayo alisema, “katika mpango mkakati wa miaka mitatu wa benki yetu, sekta hii nyeti ya wajasiriamali imepewa kipaumbele kwa namna ya kipekee kabisa ikiwemo kutoa mafunzo ya kifedha kwa wateja wetu. Takwimu zinaonyesha sekta hii inachangia takribani asilimia 30 ya pato la taifa na katika kila biashara 10, 9 ni biashara za wafanyabiashara wadogo na wakati, hivyo ni jambo la msingi sana kuhakikisha tunawawezesha.

Tangu tuanzishe rasmi warsha kama hizi mnamo mwaka 2021, benki imeshafikia wateja 300 na dhumuni kwa mwaka huu ni kufikia wateja 150. Matunda ya hiki tunachofanya yanajidhihirisha kwenye matokeo mazuri tunayoyashuhudia ikiwemo kukua kwa mikopo kwa asilimia 14%, kukua kwa amana za wateja kwa asilimia 22%Na ambacho kinazidi kutupa hamasa ni ukuaji wa faida ya benki kwa asilimia 88%, hii ni kwa kulinganisha matokeo ya Juni mwaka jana na Juni mwaka huu.” alisema Bw. Adam Mihayo.

Mkurugenzi Mtendaji aliongezea kwamba, “benki imeweza pia kua na matokeo mazuri katika mikopo chechefu na katika kipindi cha kufikia mwezi Juni benki imefikia asilimia 1.5% ya mikopo chechefu, hii ni chini ya kiwango kinachohitajika na Benki Kuu ya Tanzania cha 5%. matokeo haya yanatuambia kwamba wateja wetu ni wazuri na walipaji wazuri pia wa mikopo yao”.

Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa wateja wetu wote wa Bank of Africa Tanzania kwa kuendelea kutuunga mkono na pia natoa wito kwa wajarisiamali wa Tanzania, hususani hawa wadogo na wakati; kwamba benki ipo tayari kuhakikisha mafanikio yao, kama dhima ya warsha yetu inavyosema “TUKUE PAMOJA” benki imejizatiti kuendelea kuwekeza katika sekta hii.
 
 Hili likijieleza wazi katika mpango mkakati wa miaka mitatu wa benki yetu tukitegemea kuwekeza bilioni 88 kwa mwaka 2022- 2024, na kwa kipindi cha mwaka jana tumetoa mikopo takribani bilioni 57, huku zaidi ya bilioni 73 zikiwekezwa mwaka huu kufikia mwezi Juni. Hii inatuashiria kwamba mwaka huu tutatoa mikopo mingi kuliko mwaka jana.” alisema bwana Mihayo.

Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo na wakati, Bi. Ninael Mndeme amewahakikishia wafanyabiashara hao kwamba huduma za mikopo zitatolewa kwa wakati bila kuchelewa kwa kuzingatia kanuni za kibenki nchini.

“Kwetu sisi mteja anaweza kupata huduma za kibenki kupitia matawi yetu, lakini pia benki imejidhatiti katika uwekezaji wa huduma za kidigitali kama vile huduma za benki kwa njia ya simu (B-Mobile), huduma za benki kwa njia ya mtandao (BOAWeb-Internet Banking) na hivi karibuni tumezindua huduma ya Bank of Africa WAKALA tukiwa na zaidi ya mawakala 200 nchini kote”. Alisema Bi Ninael Mndeme.

Baadhi ya wafanyabiashara waliohudhuria warsha hiyo, wameipongeza BANK OF AFRICA kwa namna ilivyowawezesha kwa njia ya mikopo na kuinua biashara zao ambapo wameomba benki hiyo kuendelea kuboresha zaidi huduma zake ili kuwanufaisha wafanyabiashara wengi zaidi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...