Mheshimiwa  Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mobhare Matinyi  akizungumza na wafanyabiashara  wa matunza  katika ziara aliyoifanya  kwenye soko la Tazara.
Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mobhare Matinyi akiskiliza jambo  kutoka kwa mwakilishi wa wauza Matunda katika soko la Tazara Jijini  Dar es Salaam.

Na Khadija Kalili, Michuzi Tv
MKUU wa Wilaya ya Temeke Mheshimiwa Mobhare Matinyi ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Siasa Wilaya, leo Agosti 11, 2023 ameambatana na Kamati ya Siasa ya Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kufanya ziara soko la Tazara ikiwa ni katika kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa mwaka wa fedha 2022/2023.

Akiwa katika soko hilo Mhe . Matinyi ametoa wito kwa wafanyabiashara sokoni hapo kufanya usafi ili kujiepusha na magonjwa ya milipuko na kuzingatia afya za watumiaji wa soko hilo maarufu kwa kuuza matunda.

"Pamoja na mikikimikiki ya masoko ilivyo, lakini tusikubali kuishi katika hali ya uchafu, Kamati za mazingira kwenye Kata na Mitaa yetu tushirikiane kuhakikisha maeneo yetu yanakuwa safi" amesema DC Matinyi.

Aidha Mhe. Matinyi amekagua mradi wa uboreshaji miundombinu katika maeneo ya wafanyabiashara ndogondogo sokoni hapo na kusikiliza changamoto za wafanyabiashara hao ikiwemo ulipaji wa ushuru wa Manispaa.

Kaimu Mkurugenzi Wakili Faraja Nakua ameuomba uongozi wa soko hilo la Tazara kuratibu mapendekezo ya kipi kifanyike kwenye upande wa ushuru na kuahidi kuwa Halmashauri ipo tayari kukaa na kupitia kwa maslahi ya pande zote.

Usafi kwenye maeneo ya makazi na biashara ni mojawapo ya mambo ambayo DC Matinyi amekuwa akishughulikia tangu alipoteuliwa na Rais Dkt .Samia Suluhu Hassan.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...