Na Khadija Kalili Michuzi Tv
MAKAMU wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango amewasisitiza Wakuu wa Mikoa nchini kujenga maadili ya kutunza siri zote za serikali ikiwa ni moja kati ya miiko ya Uongozi.

Dkt. Mpango amesema haya leo asubuhi wakati alipokuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa mafunzo ya Uongozi kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa Tanzania Bara yaliyoanza leo Agosti 22 hadi 27 mwaka huu yanauofanyika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere iliyopo Wilayani Kibaha Mkoani Pwani .

Amesema kuwa ofisi yake imepokea malalamiko mbalimbali ikiwa ni pamoja na kushindwa kudhibiti uvujaji wa siri za serikali hasa katika kipindi hiki cha ukuaji wa teknolojia ya mitandao duniani , huku malalamiko mengine ameyataja kuwa ni mahusiano mabaya , unyanyasaji wa kingono, upendeleo wa kupandisha madaraja , uhusiano mbovu na viongozi wa Chama na Taasisi za serikali wakiwamo Taasisi ya Kuzuia na kupambana nan Rushwa (TAKUKURU) wakati wakitimiza wajibu wao wakazi.

Matumizi mabaya ya rasilimali fedha nimepataa taarifa kuwa katika mikoa Wakuu wa Mikoa hiyo wanataka kuingilia kazi za Afisa Masarufi huku baadhi ya Halmashauri, kuto shughulikia baadhi ya kero za wananchi kwa wakati hali inayopelekea wananchi kupeleka malalamiko yao kweye ngazi mbalimbali za serikali ikiwemo kuandika barua kwa viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Kero nyingine ambayo inadaiwa kuwakera wananchi kutoka kwa baadhi ya Wakuu hao wa Mikoa ni kuto wathamini wawekezaji huku wakiwakumbuka pindi wanapokuwa na shughuli zao mbalimbali ndipo huwatembezea bakuli kwa kuomba wachangiwe ikiwamo mbio za mwenge.

"Natarajia katika mada 20 ambazo nimeambiwa kuwa mtafundishwa ni pamoja na kukumbushana kuwa ninyi ndiyo wasaidizi wakuu wa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan hivyo ni muhimu kufahamu jambo hili na kuyapa kipaumbele majukumu yenu ya kazi kwa ujumla hii ni kwa mujibu wa Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2020", amesema Dkt.Mpango.

"Kukumbushana umuhimu wa rasilimali watu na rasilimali Uongozi hivyo kwa kupitia mafunzo haya mtaongeza stadi na ujuzi katika uwanda wa Uongozi" amesema Dkt. Mpango.

Mhe.Dkt.Mpango amewakemea baadhi ya Wakuu wa Mikoa hakuwataja kutokana na kupewa shutuma za kutoelewana na baadhi ya viongozi wa chama na serikali, shutuma za kujihusisha na masuala ya unyanyasaji wa kingono, kutosimamia mapato ya Mikoa yao, kuto wapandisha madaraja wanaostahili na kupandisha madaraja kwa upendeleo watumishi huku baadhi ya Wakuu wa Mikoa kuto kuwa na maelewano mazuri na Makatibu Tawala wao jambo ambalo linaleta athari katika uwajibikaji, pia amefmgusia suala la baadhi yako kuwa wababe katika utendaji wa kazi na maamuzi pia kumekuwa na udhaifu wa malalamiko ya kukosekana kwa mahusiano mazuri ya kazi baina ya baadhi ya Wakuu wa Mikoa na Wabunge, Wakurugenzi wa Halmashauri Manjspaa , Madiwani na Vyombo vingine ikiwemo Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

Malalamiko mengine yaliyotolewa kwa baadhi ya Wakuu hao wa Mikoa ni pamoja na usimamizi hafifu wa miradi ya serikali na maeneo ya utawala kutosimamiwa ipasavyo huku baadhi ya Mikoa ikiwa na kasi ndogo ya utatuzi wa kero za wananchi na kutozipatia muafaka kwa wakati.

"Jambo lingine ambalo limeonekana kuwa ni miongo mwa changamoto ni pamoja na kuwa na jitihada finyu za kuvutia wawekezaji,zingatieni maadili na nidhamu katika maeneo yenu ya kazi nendeni mkazingatie kutenda na kuongeza njia shirikishi ili kuleta maendeleo ya wananchi"amesema Dkt.Mpango.

Viongozi wengine ambao wamehudhuria ufunguzi wa mafunzo hayo ni pamoja na Mhe. Waziri wa Nchi OR -TAMISEMI Angella Kairuki ,Katibu Mkuu OR-TAMISEMI ambao ndiyo wameandaa mafunzo hayo.

Wengine ni Katibu Mkuu ,OR -TAMISEMI Adolf Ndunguru, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora (OR- MUUUB) Waziri Ridhiwani Kikwete ambaye amemuwakilisha Waziri wa Wizara hiyo Mhe.George Simbachawene.

Aliyekua Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara Mzee Philip Mangula pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Pwani.

Makamu wa Rais Dkt. Mpango amewataka Wakuu wa Mikoa hiyo kwenda kutatua vema migogoro ya ardhi kote nchini ambayo inaonekana kuwa changamoto sugu.

"Sikilizaneni jadilianeni na muelezane kwa usahihi mada zote 20 na msisite kuleta mapendekezo serikalini" Dkt. Mpango.

Katunzeni vyanzo vya maji katika Mikoa yenu sambamba na kuhifadhi mazingira, kuweni na mipango bora ya matumizi ya ardhi ili kukwepa migogoro, imarisheni ushirikiano mio ngoni mwenu na vyombo vingine,pia nawasihi someni na kuelewa nyaraka muhimu za serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM),msome ilani ya uchaguzi,mpango wa maendeleo ya taifa na sheria mbalimbali za nchi"amesema Dkt.Mpango.

Makamu wa Rais amewataka Wakuu wa Mikoa hiyo kukuza sekta binafsi katika Mikoa yao.

Waziri wa Nchi ,OR-TAMISEMI Mhe.Angella Kairuki amesema kuwa mafunzo hayo yameanza leo Agosti 22 na yatafungwa Agosti 27 na mgeni rasmi atakuwa Mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan na wawezeshaji wa mafunzo hayo ni Benki ya NMB.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaji Abubakari Kunenge amesema kuwa mafunzo haya yamekuja katika wakati muafaka " tukitoka hapa twende kujibu malalamiko ya wananchi, kutatua kero zinazowakabili kadhalika kwa upande wetu naona Mhe.Makamu wa Rais ametupa uwanja wa kuweza kutoa mapendekezo mbalimbali ambayo yataleta tija kwa taifa,pia jambo la msingi tukimaliza mafunzo haya ni kwenda kusimamia kutunza siri za serikali zisitoke nje ,tutakwenda kusimamia vyema utekelezaji wa miradi ya serikali kwani Mikoa ikiendelea ndipo nchi huendelea.

Wakati huohuo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amesema kuwa ameshkuru kupata fursa hii ya mafunzo na kusema kuwa ndani ya Mkoa wa Dar es Salam wanazingatia mgawanyiko wa kazi amesisitiza kusimamia maadili ya kazi ili.kuepusha migongano katika sehemu ya kazi "Sisi wa Dar es Salaam tunajitahidi hatuingiliani katika kazi ila ikumbukwe sisi viongozi ni wanadamu lakini kukosolewa ni lazima na tuna wajibu kama viongozi kujua dhamana tuliyoibeba baada ya kuaminiwa na Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan tunaahidi kwenda kuongeza nguvu katika sekta binafsi tutawapigania sababu wao ni katika maendeleo ya nchi na niseme wazi kwamba mafunzo haya yatakuwa nyenzo muhimu katika kazi zetu za kila siku" amesema Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Chalamila.
Makamu wa Rais Dkt.  Philip Isdor  Mpango  akizungumza  wakati akifungua mafunzo  ya Uongozi kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa Tanzania Bara  leo Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere iliyopo Wilayani Kibaha Mkoani Pwani.

Kutoka kushoto  ni  Waziri  wa Nchi OR TAMISEMI  Angella Kairuki  katikati ni Makamu wa Rais Dkt.  Philip Mpango  na Naibu Waziri  wa Nchi OR-MUUUB ,
Ridhiwani  Kikwete wakiwa wamekaa meza kuu leo kwenye ufunguzi huo mafunzo ya Uongozi  kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala  wa Mikoa Tanzania Bara.
Waziri wa Nchi  OR-TAMISEMI ,Mhe.Angella  Kairuki  akizungumza  kwenye  ufunguzi wa  mafunzo hayo  leo Agosti  22 ,2023 kwenye Shule  ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere iliyopo Wilayani Kibaha Mkoani Pwani.
Kikosi cha bendi kutoka Chuo Cha Magereza  Kibaha Mkoani Pwani  wakipumzika.mara baada ya kutoa burudani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...