Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) kimeungana na Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi katika Bonanza la Uzinduzi wa Michezo ya shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali Tanzania'SHIMIWI' ambayo hufanyika Kila mwaka.

Uzinduzi wa Bonanza hilo ni maandalizi ya Michezo ya SHIMIWI inayotarajiwa kufanyika mwezi Septemba 2023 limebebwa na Kauli mbiu isemayo "Michezo hujenga afya Bora kwa wafanyakazi" limefanyika leo Jijini dodoma ambapo Mhe. Balozi Dkt. Moses Mpogole Kusiluka, Katibu Mkuu Kiongozi alikuwa mgeni rasmi.

Watumishi kutoka Chuo cha Bahari Dar es Salaam wakiongozwa na Mwalimu wa Michezo (DMI) Ndg. Mansour Likamba na Mwalimu wa Riadha (Wizara ya ujenzi na Uchukuzi) Ndg. Samweli Pununter walipata fursa ya kuungana na watumishi wa Wizara mbalimbali na Taasisi za Serikali katika Bonanza hiloMwalimu wa Michezo DMI Ndg Mansour Likamba (Wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi.
Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...