Na Mwandishi wetu Dodoma

Moja ya Malengo ya Serikali ifikapo 2025 ni kufikia asilimia 80 ya intaneti yenye kasi katika maeneo yanayohusiana na jamii ili kuwezesha wananchi kufikia uchumi wa kidigitali pamoja na kuweka mawasiliano kuwa bora.

Kauli hiyo imetolewa na Mratibu wa Jukwaa la Usimamizi wa Intanenti Tanzania Nazar Nicholas leo Jijini Dodoma wakati wa Mkutano wa wadau wa huduma za mitandao (internet) ,na kusema moja wapo ya njia Bora na kubwa katika kupunguza Ajira za Vijana ni kuwa na intaneti yenye kasi ili kuwawezesha kushiriki uchumi wa kidigitali kuleta maendeleo nchini.

'' Ukiangalia sasa hivi vyuo vingi kila mwaka hivyo vyuo vinamwaga wanafunzi mtaani ajira ni kidogo, sasa kama ajira ni kidogo mojawapo ya njia kubwa sana ambayo inaweza ikaajiri vijana ni kutumia intaneti kwaiyo wakiwa na intaneti yenye kasi ina maana lengo la serikali la kufikisha asilimia 80 ya intaneti ya kasi inamaana kwamba inawezesha vijana pamoja wananchi kuweza kushiriki vizuri uchumi wa kidigitali''amesema Nazar

Aidha amewataka wadau wa Intanenti Nchini Tanzania kushughulikia zaidi changamoto zilizopo katika sekta hiyo ikiwemo kujadili na kuishauri serikali ili kupata ufumbuzi wa changamoto hizo.

'' Kwa wadau wa Intaneti hapa Tanzania tushughulike zaidi na changamoto hakuna sehemu hakuna changamoto kwaiyo nadhani sisi tuendele tujadili na kushauri serikali na hiyo kujadili na kuisukuma serikali nadhani kutapatikana suluhu ya hiyo changamoto''amesema Nazar

Kwa upande wake Imani Luvanda ambaye ni mshiriki wa Mkutano huo amesema manufaa ya Intaneti kasi yataleta faida juu namna ya kutumia mitandao ya kinamii kwa njia chanya pamoja na Upatikanaji wa internet imara hasa katika maeneo ya vijijini.

Mratibu wa Jukwaa la Usimamizi wa Initaneti Tanzania Nazar Nicholas akizungumza na wadau wa husuma za mtandao leo jijini Dodoma


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...