Na Said Mwishehe, Michuzi TV

MWANZILISHI wa Global Youth Empowerment Institute Amina Sanga amezindua kitabu chake cha Kijana wa tofauti ambacho kimeandikwa kwa lugha ya Kiswahili, Kingereza na Kifaransa ambacho lengo lake ni kuwawezesha vijana kuwa na malengo yenye mafanikio kimaisha.

Uzinduzi wa kitabu hicho umekwenda sambamba na kongamano maalumu lililoandaliwa na taasisi hiyo kwa lengo la kuwakutanisha vijana wa rika mbalimbali kujadli namna wanavyoweza kuwa wa tofauti wakati vijana wote duniani wakisherehekea siku ya vijana duniani.

Mgeni rasmi katika kongamano la vijana sambamba na uzinduzi wa kitabu hicho alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo pamoja na wageni waalikwa kutoka taasisi za umma na binafsi mbalimbali nchini.

 Akizungumzia kitabu hicho kwenye kongamano hilo la vijana , Amina Sanga amesema wakati wanasherehekea siku ya vijana duniani yenye kauli mbiu inayosema kumsherehekea kijana wa tofauti ameona ni vema kuja na kitabu hicho.

“Kwanini kumsherehekea kijana wa tofauti ?Kwasababu vijana wa kawaida wako wengi na wamejaa kila mahali ,lengo letu sisi ni kutengeneza vijana wa tofauti watakaoleta mabadiliko na matokeo chanya kwa taifa letu na dunia.

“Hivyo kongamano hili la vijana linakwenda sambamba na uzinduzi wa kitabu change cha 10 ambacho kinaitwa Kijana wa tofauti.Tunaposherehekea siku ya vijana duniani nimeona niunganishe na uzinduzi wa hiki kitabu kwasababu kusherehekea siku ya vijana maana yake tunasherehekea vijana watakaoleta mabadiliko

“Kwa hiyo hiki kitabu ni muongozo namna kijana anaweza akafanya vitu vya tofauti. Ndio maana tumeunganisha na kusherehekea hii siku lakini utafouti mkubwa wa hiki kitabu na vitabu vyangu vingine kipo katika lugha tatu Kiswahili, Kingereza na Kifaransa lakini.

“Pia kimebaba makundi maalum kama tunavyojua tunasherehekea siku ya vijana lakini tunajua vijana wako vijana walio katika makundi kama wasioona na wasiosikia(viziwi), hivyo hiki kitabu kimetafsiriwa kwenda kwenye maandishi ya nukta nundu  kwa ajili ya wasioona.”

Amina Sanga amesema pia kitabu hicho kipo katika lugha ya alama kwa ajili ya wale ambao ni viziwi na lengo la kufanya hivyo ni kuhakikisha vijana wote wanahusishwa.

Amesema wanaposherehekea siku ya vijana wasisherehekee vijana wachache peke yao bali hata wale ambao wako katika makundi maalum wana haki ya kusherehekea,kujifunza na kufikia malengo , kwa hiyo ndio lengo kubwa la kuandaa kitabu hicho.

Amefafanua katika kongamano hilo mwitio wa vijana umekuwa mkubwa na hiyo inaonesha vijana wameamka wanataka mabadiliko, wanataka kujifunza na ndio maana kwenye kongamano lao wamealika watu mbalimbali wanaofanya vitu tofauti.

“Kwa hiyo vijana wengi wamekuja kwasababu kuna mabadiliko ambayo wanayataka wengine wanataka kufanikiwa kiuchumi, kibiashara, kwa ujumla muamko umekuwa mkubwa .

“Ukiangalia sisi wengi vijana tunapita katika mfumo wa elimu rasmi ambao tunajifunza masomo ya kawaida ambayo ni mazuri lakini kitu ambacho tunakosa ni elimu ya ziada ukiachilia elimu ya darasani.

“Kwa hiyo hiki kitabu kimekuja kwasababu ya kuondoa hiyo gape ya kwamba vijana sasa waendelee kuipata elimu rasmi na hii elimu ambayo si rasmi.Tunaomba mashirika na taasisi kuungana nasi kuendelea kuwawezesha vijana wengi kuwa tofauti,”amesema Amina.

Kwa upande wake Waziri Mkumbo ametumia kongamano hilo kueleza Serikali hatua za mwisho za kuboresha mitaala ya elimu ili kuzalisha wahitimu kadri ya mahitaji ya soko la ajira.

Amewataka vijana kutathamini maarifa,ujuzi na uwezo walio nao huku akifafanua changamoto kubwa iliyopo vijana wengi hawana  ari ya kutafuta maarifa.

Pia amesema uadilfu ni jambo muhimu kwenye ajira na ni kilio cha wawekezaji wengi nchini kutoka nje.“Wawekezaji wengi wamelalamikia uadilifu mdogo kutoka kwa wafanyakazi hususani vijana.”







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...