Na. Damian Kunambi, Njombe

Wajumbe wa mkutano wa Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi(CCM)  wilaya ya Ludewa wamewataka viongozi wa serikali ngazi ya wilaya kuongeza nguvu katika zoezi la usajili na utambuzi wa Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA) kwani shughuli nyingi za sasa zimekuwa zikihitaji vitambulisho hivyo.

wajumbe hao wameyasema hayo katika kikao cha halmashauri kuu CCM wilaya mara baada ya kuwasilishwa taarifa ya utekelezaji wa Ilani kwa mwaka 2022/2023 wilaya humo iliyosomwa na mkuu wa Wilaya ya Ludewa Victoria Mwanziva ambapo moja  ya kipengele kilichosomwa ni juu ya mwenendo wa zoezi la vitambulisho hivyo.

Kwa mujibu wa taarifa ya mkuu huyo wa wilaya imeeleza kuwa wilaya ya Ludewa iliweka lengo la kuwafikia wananchi 3362 katika usajili na utambuzi wa watu kupitia mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA) lakini mpaka kufikia mwezi Juni mwaka huu wananchi 688 ndio waliofikiwa ikiwa ni sawa na asilimia 20 pekee ya lengo lililowekwa.

Hata hivyo wajumbe wa mkutano huo walionyesha kutoridhishwa na kasi ya utoaji vitambulisho hivyo ambapo wamewataka viongozi wa ngazi ya wilaya hiyo kuweka watendaji wa zoezi hilo katika ngazi za kata pia badala ya kufanyika kwa ngazi ya wilaya pekee.

Aidha mkuu huyo wa wilaya ameahidi kulifanyia kazi jambo hilo kwa kuongeza nguvu kazi sambamba na kuliwasilisha katika ngazi ya mkoa ili waweze kushirikiana pamoja katika kutatua changamoto hiyo.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...