Na Said Mwishehe, Michuzi TV

TIMU ya soka ya Kibangu Rangers imefanikiwa kutinha hatua ya fainali katika mashindano ya Ndondo Cup baada ya kuifunga timu ya Manispaa ya Temeke mkoani Dar es Salaam.

Katika mchezo huo uliochezwa leo Agosti 27 Uwanja wa Kinesi , timu ya Kibangu Rangers imefanikiwa kuingia hatua ya nusu baada ya kuiondoa timu ya Manispaa ya Temeke kwa mikwaju ya penalt baada ya dakika 90 za mchezo kumalizika kwa kufungana bao 1-1.

Baada ya kumalizika kwa bao 1-1, timu hizo ziliingia hatua ya mikwaju ya penalty ambapo Kibangu Rangers ilifanikiwa kuibuka kidedea kwa kupata penalt 4 dhidi ya penalt 3 za timu ya Manispaa ya Temeke.

Matokeo hayo yameifanya Kibangu Rangers kuingia fainali huku mashabiki wa timu hiyo waliokuwepo uwanjani hapo walionesha furaha zao kwa ushindi ambao timu yao umeipata.

Katika uwanja wa Kinesi baada ya mwamuzi kupiga filimbi ya mwisho kuashiria kumaliza mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa, ndio mashabiki walipoamua kuingia katikati ya uwanja na kuanza kushangilia huku wengine wakisakata muziki.

Hata hivyo baadhi ya wadau wa soka nchini waliokuwepo uwanjani hapo wametumia nafasi hiyo kuwapongeza waandaaji wa mashindano ya Ndondo Cup kwani mbali ya kutoa burudani yameendelea kuibua vipaji.

Kwa upande wake mdau wa soka Privadinyo amesema mashindano ya Ndondo Cup yameendelea kuwa mfano wa kuigwa katika nchi za Afrika Mashariki na baadhi ya nchi wamekuwa wakiandaa mashindano yanayofanana na hayo.

“Mashindano ya Ndondo Cup yamekuwa ni mfano wa kuigwa, wote tunakumbuka zamani mtaani Ndondo Cup ikichezwe refa anapanga wahuni wameshika mawe.Siku hizi Ndondo Cup watu wameshika vuvuzela.

“ Ndondo Cup ni mashandano makubwa yenye hadhi ya kipekee , Kenya kuna rafiki yangu ambaye ni mtangazaji wa redio anaitwa Rashid Abdallah ameanzisha mashindano kama haya , yanafanana na Ndondo Cup.”

Akizungumzia mchezo wa leo Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke Elihuruma Mabelya amesema ameshuhudia mchezo mzuri wa nusu fainali kati ya timu ya Temeke Manicipal na timu ya Kibangu Rangers kwenye mashindano ya Ndondo Cup.

“Niwashukuru Clouds kwa kaundaa mashindano haya , wamekuwa wakiandaa kila mwaka na tumeendelea kushuhudia maboresho zaidi kama tunavyoona leo,”amesema huku akisisitiza mashindano hayo yamekuwa chachu kubwa kwa vijana.

Amesema lugha nzuri ya kuzungumza na vijana ni kupitia michezo n asanaa huku akifafanua leo vijana wamekusanyika kwasababu ya michezo na hiyo ndio dhamira ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kutaka kuona vijana wanafika mbali kwenye mchezo wa soka.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke Elihuruma Mabelya akizungumza kuhusu mashindano ya Ndondo Cup

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...