Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba nchini Tanzania (TMDA), Dkt. Adam Fimbo akizungumza katika Uzinduzi wa Mradi wa Breedime uliofanyika leo tarehe 4/8/2023 katika Hotel ya Landmark Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi kutoka nchini Sweden, Karolinska Institute Stockholm, Profesa Eleni Aklillu akizungumzia mradi wa Breedime katika uzinduzi uliofanyika leo tarehe 4/8/2023 katika Hotel ya Landmark Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji Wakala wa Chakula na Dawa Zanzibar (ZFDA) Dkt. Burhani Simaia akizungumza katika Uzinduzi wa Mradi wa Breedime uliofanyika leo tarehe 4/8/2023 katika Hotel ya Landmark Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu Taasisi ya Utafiti wa Afya Zanzibar (ZAHRI) Dkt. Mayassa Ally akizungumzia Mradi wa Breedime namna utakavyowasaidia katika utendaji wa majukumu yao.
Mwakilishi wa Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS). Profesa Elianginlingo Kaole akizungumza namna watakavyotumia fursa ya mradi Breedime katika kuzalisha wahitimu bora wa uthibiti ubora Kanda ya Mashariki.







Washiriki kutoka taasisi mbalimbali wakiwa katika Uzinduzi wa Mradi wa Breedime uliofanyika leo tarehe 4/8/2023 katika Hotel ya Landmark Mbezi Beach Jijini Dar es Salaam.

Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba nchini Tanzania (TMDA) kwa kushirikiana na nchi ya Rwanda, Sweden na Uingereza imezindua mradi wa Breedime ambao unakwenda kusaidia kujenga Mifumo ya Udhibiti Ubora wa Majaribio ya Dawa.

Akizungumza leo tarehe 4/8/2023 jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa mradi wa Breedime, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba nchini Tanzania (TMDA), Dkt. Adam Fimbo, amesema kuwa mradi huo unakwenda kuongeza ufanisi katika mifumo ya majaribio ya daw Dkt. Fimbo amesema kuwa majaribio ya dawa ni tafiti ambazo zinafanyika kwa binadamu katika kupima ubora, usalama pamoja na ufanisi wa dawa kabla ya kuanza kutumia rasmi.

“Tumepata ufadhili wa fedha euro laki nne na nusu kutoka Shirika la Umoja wa Ulaya kupitia mradi huu Breedime kwa ajili ya kuendelea mifumo ya udhibiti ubora” amesema Dkt. Fimbo.

Dkt. Fimbo amesema kuwa TMDA imeendelea kufanya kazi kwa mujibu wa sheria na kupokea maombi kutoka kwa watafiti mbalimbali kwa ajili ya majaribio ya dawa.

Ameeleza kuwa wamekuwa wakipokea maombi na kuyafanyia tathmini pamoja na kutoa vibali kwa ajili ya kufanya tafiti. “Tunafanya hivyo kwa sababu dawa unampa binadamu kwa mara ya kwanza kwa ajili ya matumizi ya dawa ambazo zinakemikali”

Amesema kuwa katika sekta ya dawa lazima umefanye majaribio ya kwanza na ikibainika inaufanisi inapata kibali kwa ajili ya matumizi ya binadamu.

“Moja ya majukumu ya TMDA ni kupitisha majaribio kabla ya dawa kutumika nchini, hivyo tunapaswa kulisimamia hilo kwa uangalifu, uhadilifu mkubwa na ukikosea inaweza kuleta madhara” amesema Dkt. Fimbo.

Amesema kuwa mradi unakwenda kujenga mifumo thabiti ambao unahitaji wataalam wa kutosha wa kufanya tathmini, utaratibu wa kufanya ukaguzi katika maeneo ambapo ukaguzi unafanyika.

Ameeleza mifumo ya majaribio ya dawa inaitaji rasilimali fedha za kutosha kwa ajili ya kufanya uwekezaji wa kutosha ambao utasaidia kupitisha majaribio vizuri.

Dkt. Fimbo amesema kuwa mradi huo utafanyika kwa muda wa miaka mitatu kuanzia mwaka huu ambao unakwenda kutekeleza kwa ushirikiano baina ya nchi zinazoendelea pamoja na zile zilizoendelea.

Mkurugenzi Mkuu Taasisi ya Utafiti wa Afya Zanzibar (ZAHRI) Dkt. Mayassa Ally, amesema kuwa kupitia mradi wa Breedime utawasaidia katika kuwajengea uwezo katika kusimamia maadili ya utafiti ili waweza kufanya kazi zao kwa uweledi.

Mkurugenzi Mtendaji Wakala wa Chakula na Dawa Zanzibar (ZFDA) Dkt. Burhani Simai, amesema kuwa mradi unakwenda kuwasaidia kuzuia majanga katika utekelezaji wa majukumu yao.

Mwakilishi wa Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS). Profesa Elianginlingo Kaole, amesema kuwa wamejipanga kushiriki kikamilifu katika mradi kwa kutumia fursa hiyo kuendesha mafunzo na kuendelea kuzalisha wahitimu bora katika kozi ya Uthibiti ubora Kanda ya Mashariki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...