Na Rahima Mohamed, Sheha Sheha   Maelezo       1/8/2023

Maafisa habari wametakiwa kutumia vyombo vya habari vya serikali kutoa taarifa za utekelezaji katika  taasisi zao kwa jamii.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Habari na Matukio kutoka shirika la Utangazaji Zanzibar Salum Ramadhan kwa niaba ya Mkurugenzi wa Shirika hilo katika mkutano wa maafisa habari, mawasiliano na uhusiano wa taasisi za Serikali huko Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Mkoa wa Mjini Unguja.

Amesema maafisa kuna umuhimu mkubwa kwa viongozi wa taasisi za umma kutumia vyombo vya habari ili wananchi wajue maendeleo yanayofanywa na serikali yao.

Aidha amesema maafisa habari wanatakiwa kutumia njia mbalimbali kutoa taarifa  katika taasisi zao ikiwemo kuandaa Makala, matangazo  na vipindi mbali mbali vinazotoa uchambuzi  zinazoeleza maendeleo ya nchi.

Vilevile, amewashajihisha maafisa habari hao  kuvitumia vipindi vya asubuhi njema na dira vinavyoendeshwa na shirika hilo ambavyo vinatoa nafasi kwaviongozi wa taasisi mbali mbali kuzungumza na Wananchi.

Mkurugenzi Salum ameipongeza Idara ya habari Maelezo  kwa  kusimamia sera ya habari  na kuwakutanisha pamoja  maafisa hao kwa lengo la kujua maendeleo wanayoyafanya na changamoto wanazokumbana nazo katika majukumu yao ya kila siku.

Mkurugenzi wa idara ya Habari Maelezo amewataka wakuu wa taasisi mbalimbali kuwashirkisha maafisa Habari katika kazi zao ili jamii iweze kuhabarika juu ya kazi hizo.

 Aidha amewataka maafisa habari kuwa wabunifu  katika kuandaa kazi zao za kihabari na kuendana na kasi teknolojia ya habari na mawasiliano.

 

Kwa upande wao maafisa habari kutoka taasisi mbali mbali, wamesema kumekuwa na changamoto mbali mbali ambazo zinarejesha nyuma majukumu yao ipasavyo ikiwemo ufinyu wa bajeti na ushirikishwaji mdogo.


Mkurugenzi Habari na Matukio wa Shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC Salum Ramadhan Abdalla akitoa hotuba katika Mkutano wa Maafisa Habari,Mawasiliano na Uhusiano uliofanyika katika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar.

Afisa Habari wa ZRA Makame Khamis akitoa Taarifa ya Jumuia ya Maafisa Habari wa Serikali katika Mkutano wa Maafisa Habari,Mawasiliano na Uhusiano uliofanyika katika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar.

Afisa Uhusiano Mkoa wa Kaskazini Shaame Siami kitoa Mchango wake katika Mkutano wa Maafisa Habari,Mawasiliano na Uhusiano uliofanyika katika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...