Na Mwandishi Wetu

BOHARI ya Dawa (MSD) imejipanga kuboresha huduma zake na kuongeza uwezo wa kuhifadhi bidhaa za afya, ili kuendana na kasi ya Serikali ya ujenzi wa hospitali na vituo vya afya, sambamba na ongezeko la idadi ya watu.

Akizungumza wakati wa makabidhiano ya michoro na eneo ujenzi wa ghala la kisasa la kuhifadhi dawa kwa ajili ya Kanda ya MSD Mtwara baina ya MSD Na Kampuni ya Hainnan International,  Meneja Miradi Msonge wa MSD, Elias Masumbuko amesema wameshuhudia maboresho makubwa sekta ya afya.

"Tumeendelea kushuhudia maboresho makubwa ya sekta ya afya chini ya Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dk.Samia Suluhu Hassan katika kuongeza vituo vya kutolea huduma za afya,  hivyo MSD tunatakiwa kuwezesha vifaa na bidhaa za afya kwenye  vituo hivyo, ili kukamilisha maboresho haya, " amesema Masumbuko

Amefafanua Kanda ya MSD Mtwara, imekua na ongezeko la vituo vya afya kwa wastani kutoka 592 vya awali hadi kufikia 631, ziko hospitali nyingi zilizofanyiwa maboresho, hivyo kupelekea uhitaji wa kuhuisha uwezo wa Kanda hiyo kuhifadhi bidhaa.

Kwa upande wake  Meneja Miradi wa MSD Deo Orauya  amesema kiutaratibu MSD inatakiwa kuwa na uwezo wa kuhifadhi bidhaa kwa kiwango zinazo tosheleza miezi tisa (9), na kiwango cha chini kwa miezi mitatu (3).

"Kutokana na ufinyu wa ghala la Mtwara, Kanda hiyo inashindwa kuhimili uhifadhi bidhaa hata kwa kiwango cha chini cha miezi mitatu, na kulazimu magari ya bidhaa kusafiri kila mwezi kuleta bidhaa, hivyo kuongeza gharama za uendeshaji."

Aidha amesema MSD imemkabidhi mkandarasi Hynnan International, eneo lenye ukubwa wa ekari 30, kwa ajili ya ujenzi wa ghala la kisasa lenye ukubwa wa mita za mraba (sqm) 5,000.

Awali  Mshauri Mwelekezi wa mradi huo, kampuni ya ABECC, inayomilikiwa na Chuo Kikuu cha Ardhi Dar es salaam, imeahidi weledi katika kushauri na kumsimamia Mkandarasi huyo ili kuhakikisha ujenzi huo unakamilika ndani ya muda uliopangwa, ambao mwaka mmoja.















 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...