Na Janeth Raphael - Michuzi Tv - Dodoma.

Imeelezwa kuwa kwa mwaka wa fedha 2023/2024 Serikali imeitengea Bohari ya Dawa Nchini Tanzania (MSD) kiasi cha shilingi bilioni 205 kwa ajili ya ununuzi wa bidhaa za afya.

Pia kuimarisha upatikanaji wa bidhaa za afya na miundombinu ya utunzaji wa ambapo Ujenzi wa maghala unatarajiwa kuanza rasmi mwezi wa 8 mwaka huu.

Kauli hiyo imetolewa leo na Meneja Mipango, Ufuatiliaji na Tathimini  wa Bohari ya Dawa ( MSD)  Hassan Ibrahim akizungumza na wanahabari kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Bohari na muelekeo wake kwa mwaka wa fedha 2023/2024 katika ukumbi wa Idara ya Habari-MAELEZO jijini Dodoma.

Hassan amesema kuwa bohari itaanza uzalishaji wa mipira ya mikono kwa kiwanda kilichopo kijiji ch Idofi, Mkoani njombe.

Pia kiwanda kitatekeleza miradi ya uzalishaji wa viwanda vya bidhaa za afya eneo la Zegereni, Mkoani Pwani na uzalishaji wa viwanda vya pamba tiba. 

"MSD ipo kwenye maandalizi ya awali ya kutekeleza mradi wa ujenzi wa kiwanda Cha kuzalisha dawa na bidhaa za pamba tiba" - Hassan

Aida Hassan amesema kuwa MSD ina mpango wa kujenda maghala ya kisasa katika Mikoa ya Dodoma, Mtwara na Kagera Kwa lengo la kuongeza nafasi zs kuhifadhi bidhaa na kuimarisha ubora wa bidhaa za afya.

Hata hivyo Serikali kupitia bohari ya dawa imefunga mitambo miwili ya kisasa kwenye eneo la Bohari ya dawa keko Mwanga, Dar es salaam Kwa ajili ya kuzalisha aina mbili za barakoa maalum aina ya N95 zenye uwezo wa kuzuia maambukizi hatarishi ya njia ya hewa na chembe chembe za vumbi la viwandani na kwenye migodi vyenye uwezo wa kuzalisha barakoa milioni 10.8 kwa mwaka.

Meneja Mipango Ufuatiliaji na Tathimini wa Bohari ya Dawa Nchini (MSD) Hassan Ibrahim akizungumza na wanahabari kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Bohari ya Dawa Nchini Tanzania na muelekeo wake kwa mwaka wa fedha 2023/2024 Katika ukumbi wa idara ya habari-MAELEZO ijini Dodoma leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...