Na Janeth Raphael -MichuziTv - Dodoma

Ili kukabiliana na uharibifu wa visumbufu vya mazao mashambani Serikali imeanza rasmi kutumia Ndege zisizo na rubani (Drones)huku ikisisitiza wakulima wanakwenda kufanya kilimo chenye tija na ufanisi katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

Wizara ya Kilimo imekutana pamoja na wadau wa Shirika la Kimataifa la Mpango wa chakula Duniani (WFP),kwa ajili ya kujadili kuunda kituo kimoja cha kupokea taarifa,kufuatilia ikiwemo kudhibiti visumbufu hivyo vya mazao shambani.

Hayo yamezungumzwa na Waziri wa Kilimo Hussein Bashe wakati wa hafla ya kupokea Drones kubwa yenye uwezo wa kupulizia dawa na viuatilifu katika hekta 20 kwa saa moja,pamoja na Vishkwambi 370 vyenye thamani ya sh Milion 364.

Waziri Bashe amesema vifaa hivyo ni muhimu sana katika Sekta ya Kilimo kwa sababu Drone hiyo kubwa kuliko nyingine ambayo syerikali inayo inakwenda kuwa suluhisho la visumbufu vya mazao katika mashamba.

"Nawashkuru sana WFP kwa kutupatia vifaa hivi, ambavyo Vishkwambi vinakwenda kugawiwa kwa Maafisa Ugani kwa ajili ya kukusanya taarifa mbalimbali za Kilimo,"amesema Bashe.

Aidha Badge amesema,kwa kuanzia kupitia vifaa hivyo wanakwenda kupima mashamba ya vijana wa program ya BBT ili kuona kama yana visumbufu vya mazao ili waweze kuvidhibiti kabla hawajaanza kulima.

"Tunashkuru sana ushirikiano unaofanywa na wadau wa mbalimbali wa Kilimo kutupatia vifaa inaonyesha jinsi gani wadau wanavyounga mkono jitihada za serikali katika kukuza kilimo hapa nchini,"alisema Bashe.

Akizungumzia kuhusiana na kuketu pamoja na WFP kwa ajili ya kuunda kituo kimoja cha kupokea taarifa na kufuatilia ikiwemo kudhibiti visumbufu vya mazao mashambani,alisema wamefikia hatua nzuri ya mazungumzo.

"Kwa sababu tumekuwa na Drones nyingi,tumepanga kuanzisha kituo kimoja kwa ajili usimamizi wa Drones hizo ikiwemo kufuatilia taarifa za visumbufu vya Mazao,"alisema Bashe.

Kwa upande wake Mwakilishi Mkazi wa WFP Sarah Gibson alisema amefurahishwa na ushirikiano aliopewa na wizara hiyo huku akiahidi kuendeleza ushirikiano na serikali ili kuhakikisha wanakuza na kuendeleza shughuli za Kilimo.

"Tutaendelea kushirikiana na serikali ili kuhakikisha kilimo kinapiga hatua zaidi,na hii kuunga mkono jitihada za serikali katika kuboresha kilimo,"alisema Gibson.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Afya ya Mimea (TPHA) Profesa Joseph Ndunguru alisema vifaa hivyo vimekuja wakati muafaka hasa ukizingatia tunaelekea kwenye msimu wa kilimo.Kutokana hilo alisema wakulima wategemee kufanya kilimo chenye tija ambacho kitawainua kiuchumi.





 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...