Na Mwandshi Wetu-DODOMA.
Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma PPRA imezitaka Taasisi zote za Umma nchini kuhakikisha zimepatiwa mafunzo elekezi kwa ajili ya utumiaji wa Mfumo mpya wa Ununizi wa Umma kwa njia ya mtandao (NeST).
Hayo yamesemwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA Bw. Eliakim Maswi wakati akiendesha mafunzo kwa wafundishaji (ToT) juu ya matumizi ya mfumo wa NeST jijini Dodoma hivi karibuni.
Bw. Maswi amesema kuwa katika kukamilisha mpango wa Serikali wa kupata thamani ya fedha katika ununuzi wa umma Taasisi zote za umma zinatakiwa kuhakikisha watendaji wake wote waliopo kwenye mnyororo wa ununuzi wanapatiwa mafunzo elekezi juu ya utumiaji wa mfumo wa NeST.
“Niwaombe Wakurugenzi wa Halmashauri na Wakuu wa Taasisi nyingine za Umma kuhakikisha wanaleta watu wao kwenye mafunzo ya matumizi ya mfumo, na isitoshe tu kuwa watu bali ni watu wenye upeo mpana wa kuelewa, kwa sababu kupitia wao tunataka wakawe msaada kuwafundisha wengine namna ya kutumia mfumo huu”
Aidha Bw. Maswi ameweka bayana juu ya hatua za kisheria zitakazochukuliwa dhidi ya taasisi ambazo zitakwepa kutumia mfumo katika michakato ya kufanya ununuzi kuwa Sheria itatoa adhabu ya faini ya kiasi kisichopungua Shilingi milioni kumi. Kwani kufanya hivyo ni kuzorotesha juhudi za Serikali katika mpango wa kuleta maendeleo hususan katika Sekta ya ununuzi.
“ Sheria itatoa adhabu ya kutozwa kiasi cha fedha kisichopungua milioni kumi kwa Taasisi yoyote ambayo itaendesha shughuli za ununzi nje ya mfumo” Alisema Bw, Maswi.
Mafunzo hayo yanayotarajiwa kuendeshwa ndani ya siku tano yamehusisha jumla ya washiriki zaidi ya 160 kutoka katika Mikoa 26 na Halmashauri ikiwa kila Halmashauri zilizoshiriki zikitoa wawakilishi 6 wanaopatiwa mafunzo kwaajili ya Kwenda kuwafundisha watendaji wengine.
Kwa upande wake Mgeni rasmi wa mafunzo hayo Katibu Mkuu TAMISEMI Bw. Adolf Ndunguru naye amesisitiza kuwa Taasisi za umma zinatakaiwa kuendelea kuwataka wazabuni wao kujisajili kwenye mfumo wa NeST kwani bila kufanya hivyo malengo ya kutolewa mafunzo hayo hayatafikiwa kwani bila ya wazabuni kujisajili lengo la kuendesha mchakato wa ugawaji wa zabuni za umma halitafikiwa.
“Nitoe wito kwenu nyinyi na Taasisi nyingine za umma kuendelea kuwasisitiza wazabuni kujisajili katika mfumo, kwani bila ya wao hiki tunachokifanya hapa ni bure”
Muendelezo wa utoaji wa mafunzo Hayo elekezi ni maandalizi ya kuwajengea uwezo watumiaji wa mfumo huo mpya wa NeST ambao ni Taasisi zote za umma na wazabuni, ambapo mpaka ifikapo Septemba 30 hakuna taasisi yoyote ambayo itaruhusiwa kutangaza zabuni nje ya mfumo wa NeST.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...