Taasisi ya elimu Tanzania TET na Kituo cha Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika wametia Saini ya hati ya makubaliano ya Uendelezaji hitoria ya Ukombozi wa Bara la Afrika ambapo watashirikiana katika kuandaa maudhui ya historia ya ukombozi na kuingizwa kwenye vitabu vya kiada na ziada.

Hafla ya utiaji Saini wa Makubaliano hayo iliyofanyika leo Agosti 11, 2023, imeshuhudiwa na Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Balozi Pindi Chana ambapo pamoja na mambo mengine, pia makubaliano hayo yamelenga kutoa mafunzo kwa Walimu waliopo kazini na Walimu tarajali waliopo vyuoni ambayo yatawawezesha kutumia njia mbalimbali katika kufundishia.

Akizungumza mara baada ya makubaliano hayo Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda amesema ni muhimu Tanzania ikahifadhi historia ya ukombozi wa Bara la Afrika, ili vizazi vijavyo vitambue namna ambavyo Viongozi wa Nchi ya Tanzania walivyopambania uhuru wao na wa Mataifa mengine ya Bara la Afrika.

“Tusipojua tulipotoka, hatutajua tunapoenda na historia ya urithi wetu itapotea, njia ya kwanza ya kujua sisi kama watanzania, Kama wana Bara la Afrika lazima turudi nyuma tujue tulipotoka, harakati za ukombozi ni muhimu, kumbukumbu ambazo zinatunzwa hapa ni muhimu kwa Bara la Afrika na ni muhimu kwa vizazi vyetu, ni muhimu kujua kuwa Tanzania iliongoza harakati za ukombozi ni muhimu watu wetu wajue, kulikuwa na ubaguzi wa rangi na elimu.” amesema Profesa Mkenda.

Profesa Mkenda amesema ni muhimu vitabu vya urithi wa ukombnozi vichapishwe kwa wingi na kusambazwa katika mashule na maktaba mbalimbali ili watanzania na watu wa Afrika wajue thamani ya ukombozi wa nchi zao.

Kwa upande wake Waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo Balozi Dkt. Pindi Chana amesema makubaliano hayo yamekuja wakati muafaka kwani Wizara yake na Wizara ya Elimu walishaanza mazungumzo kuhusu kuingizwa kwa program za historia ya urithi wa ukombozi katika mitaala hiyo lengo likiwa ni kuelezea Tanzania ilifanya nini katika kusaidia nchi nyingine kupata uhuru.

“Utiaji Saini uliofanyika hapa tulishajadiliana sana wakati wa Bunge, sisi tulishaanza mazungumzo kwamba katika mitaala yetu tutaweka program za urithi wa ukombozi, hata kwenye michezo tukasema tutaweka mitaala hii ya urithi wa ukombozi ili watu wote wajue Tanzania ilifanya nini katika kusaidia nchi zingine, kwa hiyo historia ni lazima kuitunza katika maktaba zetu, janga linalotutafuna ni kutokuelewa historia yetu, lazima tuwe na maadili, lazima tuwe na taifa lenye utamaduni unaoeleweka, lugha yetu ya kiswahili, muarobaini wake ni hii leo ni lazima tuwe na vitabu vinavyoonesha historia yetu ya Tanzania katika Ukombozi wa Bara la Afrika” Amesema Balozi Dkt. Chana.

Nae Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania TET Dkt. Aneth Komba amesema makubaliano hayo yanahusu kuhifadhi urithi wa ukombozi kwenye kuandaa vitabu vinavyoelezea kumbukumbku ya ukombozi wa Bara la Afrika na kuingizwa kwenye mitaala ya kaunzia darasa la nne pamoja na kutoa mafunzo kwa walimu yatakayowezesha wanafunzi kujua historia ili kuwa na kizazi cha wanafunzi ambao ni weledi katika kutunza na kuenzi, na kujivunia historia ya Bara la Afrika.

“Tumekubaliana kushirikiana katika kuandaa, kuhuisha maeneo mbalimbali ya maeneo ya uhuishaji wa ukombozi wa bara la Afrika, maudhui ya historia ya ukombozi wa Bara la Afrika yameanza kuingizwa kuanzia vitabu vya dara la nne ambayo yanahusisha katika kuandaa vitabu vya kiada na ziada, tutajitahidi kuhakikisha kunakuwa na vitabu vya ziada vya kutosha na tutawahamasisha wachapaji waje kuchukua maudhui ya kutosha” amesema Dkt. Komba.

Katika Hafla hiyo Mratibu wa Kituo cha Urithi wa Ukombozi wa Ukombozi wa Bara la Afrika Bw. Boniface Kadili amesema kituo hicho kina maudhui ya kutosha kuwawezesha wanafunzi kufahamu kwa ukubwa mchango wa Tanzania kwa mataifa ya Bara la Afrika ya kupata uhuru wao.
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Balozi Pindi Chana wakishuhudia utiaji saini hati ya makubaliano ya Uendelezaji hitoria ya Ukombozi wa Bara la Afrika kati ya Taasisi ya elimu Tanzania TET na Kituo cha Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika ambapo watashirikiana katika kuandaa maudhui ya historia ya ukombozi na kuingizwa kwenye vitabu vya kiada na ziada. Hafla hiyo imefanyika leo Agosti 11,2023 katika Ofisi za Kituo cha Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika Jijini Dar es Salaam.


Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda akimsikiliza Mratibu wa Kituo cha Urithi wa Ukombozi wa Ukombozi wa Bara la Afrika Bw. Boniface Kadili alipowasili kwaajili ya kushuhudia hafla ya utiaji saini hati ya makubaliano ya Uendelezaji hitoria ya Ukombozi wa Bara la Afrika kati ya Taasisi ya elimu Tanzania TET na Kituo cha Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika ambapo watashirikiana katika kuandaa maudhui ya historia ya ukombozi na kuingizwa kwenye vitabu vya kiada na ziada. Hafla hiyo imefanyika leo Agosti 11,2023 katika Ofisi za Kituo cha Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda pamoja na Waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo Balozi Dkt. Pindi Chana wakicheza mchezo wa bao wakati walipowasili kwaajili ya kushuhudia hafla ya utiaji saini hati ya makubaliano ya Uendelezaji hitoria ya Ukombozi wa Bara la Afrika kati ya Taasisi ya elimu Tanzania TET na Kituo cha Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika ambapo watashirikiana katika kuandaa maudhui ya historia ya ukombozi na kuingizwa kwenye vitabu vya kiada na ziada. Hafla hiyo imefanyika leo Agosti 11,2023 katika Ofisi za Kituo cha Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini hati ya makubaliano ya Uendelezaji hitoria ya Ukombozi wa Bara la Afrika kati ya Taasisi ya elimu Tanzania TET na Kituo cha Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika ambapo watashirikiana katika kuandaa maudhui ya historia ya ukombozi na kuingizwa kwenye vitabu vya kiada na ziada. Hafla hiyo imefanyika leo Agosti 11,2023 katika Ofisi za Kituo cha Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika Jijini Dar es Salaam.Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Balozi Pindi Chana akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini hati ya makubaliano ya Uendelezaji hitoria ya Ukombozi wa Bara la Afrika kati ya Taasisi ya elimu Tanzania TET na Kituo cha Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika ambapo watashirikiana katika kuandaa maudhui ya historia ya ukombozi na kuingizwa kwenye vitabu vya kiada na ziada. Hafla hiyo imefanyika leo Agosti 11,2023 katika Ofisi za Kituo cha Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania TET Dkt. Aneth Komba akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini hati ya makubaliano ya Uendelezaji hitoria ya Ukombozi wa Bara la Afrika kati ya Taasisi ya elimu Tanzania TET na Kituo cha Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika ambapo watashirikiana katika kuandaa maudhui ya historia ya ukombozi na kuingizwa kwenye vitabu vya kiada na ziada. Hafla hiyo imefanyika leo Agosti 11,2023 katika Ofisi za Kituo cha Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...