Serikali kupitia kituo cha uwekezaji Nchini –TIC kimewasihi mabalozi wa Tanzania katika Nchi mbalimbali kujikita katika kutafuta fursa za uwekezaji na kuangalia maeneo ambayo kama Nchi yatanufaika nayo ikiwemo sekta ya Viwanda.

Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa idara ya uhamasishaji  uwekezaji –TIC, John Mnali katika mafunzo na mabalozi wa Nchi mbalimbali ambao wameapishwa na kupangiwa vituo hivi karibuni na Rais Dkt Samia Suluh Hassan.

Kuhusu maeneo ya uwekezaji Mnali amesema serikali imetenga maeneo ya kutosha kwa ajili wawekezaji ikiwemo kongani la viwanda lililopo wilayani Kibaha Mkoani Pwani pamoja na maeneo mengine kwa kushirikiana na Halmashahuri.

Kwa upande wao baadhi ya mabalozi walioshiriki kikao hicho wamesema kuwa mafunzo hayo yatawasaidia kutafuta wawekezaji katika sekta mbalimbali ili kuleta tija kwa Taifa.

Mabalozi waliopatiwa mafunzo na –TIC ni pamoja na Balozi Joseph Sokoine Nchini Canada, Balozi Fatma Rajab Nchini Oman, Balozi Naimu Azizi Nchini Australia, Balozi Ali Mwadini Nchini Ufaransa pamoja na Na Balozi Ceasar Waitara Nchini Namibia.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...