KAMPUNI ya Vanilla International Limited imeanzisha mradi wa vanilla village mombasa katika mji mdogo wa mariakani nchini Kenya

Mkurugenzi wa Vanilla International Limited, Simon Mnkondya amechukua uamuzi huo baada ya kuona wakenya wengi wanachangamkia fursa katika kilimo cha Vanilla kuliko hata watanzania licha ya kwamba wamekuwa wakifanya mradi kama huo katika maeneo ya Arusha, Zanzibar na Katika kijiji cha Vanilla jijini Dodoma.

Mnkondya amesema ni wakati sahihi kwa wakenya kuanza kilimo cha vanilla kwa mfumo wa mashamba shufwaa yaani ‘block farming’ ili kupunguza gharama za uwekezaji, kwa ajili ya usalama na kwa ajili ya kuhakikisha uwepo wa soko la vanilla.

Vanilla International Limited itafanya mradi ikishirikiana na taasisi ya MRM foundation na Karibuni foundation zote za nchini kenya na taasisi ya Society Watch ya Tanzania.

Lengo la mradi wa Vanilla Village Kenya ni kukuza uchumi wa wakenya na waafrika kwa ujumla kwa sababu bei ya vanilla imewahi kufikia mpaka dola za kimarekani 500$ takribani 1,000,000/= ya kitanzania.

Pia kampuni imetangaza namba ya +255629300200. kenya +254 759604040

washirika:
Mkurugenzi wa Nyali Cinemax, Mr. Dipan Shah amesema Vanilla India imewafanya wakulima wawe matajiri kwa maana ni zao la pili kwa bei duniani .

Kwa Upande wa Raisi wa Upendo Foundation, Mr.Bruno Cern'o mwenye asili ya Italia amesema kwa vile Vanilla ni zao la bei kubwa ni vyema sasa waafrika kulima vanilla ili kupata utajiri endelevu na kuwa na unafuu wa maisha.

Pia Mr.Gianfranco Ranieri ambaye ni Rais wa karibuni Assogiocattoli ya Milano Italia amesema atalima heka zaidi ya 100 hapa kenya na anaenda kulima vanilla kama kicha na atakuwa kichaa wa vanilla nchini kenya.

Kwa Uapande wa Meneja Mkazi wa MRM Foundation, mama Siprosa Rabach amesema lazima Vanilla ilimwe kenya ili watu wapate kazi na utajiri kenya.
Picha ya pamoja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...