Mtafiti na Mchambuzi kutoka Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Zainabu Mmari akitoa mafunzo kwa washiriki asasi za kiraia na vituo vya Taarifa na maarifa kutoka maeneo mbalimbali hapa nchini kuhusu masuala ya jinsia na jinsia pamoja na kupanga Bajeti wakati wa mafunzo ya Bajeti yenye mrengo wa kijinsia na ufuatiliaji wa vituo vya Taarifa na maarifa pamoja na asasi za kiraia.
Mwezeshaji kutoka Idara ya Mafunzo na Ujengaji Uwezo wa Mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP), Anna Sangai akitoa elimu kuhusu mpango wa Bajeti yenye mrengo wa jinsia na ufuatiliani wa vituo vya Taarifa pamoja na asasi kwa washiriki kutoka asasi za kiraia na vituo vya Taarifa na maarifa kutoka maeneo mbalimbali hapa nchini.
Mratibu wa Vituo vya Taarifa na maarifa kutoka TGNP, Jacqueline Mtesha akizungumza kuhusu kazi zinazotakiwa kufanya Vituo vya Taarifa na maarifa kwa washiriki kutoka asasi za kiraia na vituo vya Taarifa na maarifa kutoka maeneo mbalimbali hapa wakati wa mafunzo hayo yalitofanyika katika ofisi zake zilizopo Mabibo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki kutoka vituo vya Taarifa na maarifa pamoja na asasi za kiraia wakijadiliana kwenye makundi kuhusu kitu walichokifanya kama asasi au vituo ili kuja na masuluhisho kwenye masuala ya usawa wa kijinisa kwenye mafunzo ya ya Bajeti yenye mrengo wa kijinsia na ufuatiliaji wa vituo vya Taarifa na maarifa pamoja na asasi za kiraia.
Mwenyekiti wa Kituo cha taarifa na Maarifa cha Mabibo, Neema Mwinyi akizungumza kuhusu Vituo vya taarifa na Maarifa mkoa wa Dar es Salaam ambapo vituo mbalimbali vimefanya Uchechemuzi na Ushirikishwaji wa Jmaii ambapo matokeo yaliyopatikana katika KC ya Mabibo limejengwa Daraja baada ya uchechemuzi, KC ya Saranga wamefanikiwa kuhamashisha wananchi kujenga msingi wa Zahanati ambapo baada ya jitihada hizo Serikali iliingilia kati, KC ya Kitunda wamefanikiwa kujenga ukuta kwenye Shule ambazo zilikuwa zinasumbuliwa na Panya Road, watoto kubakwa na kuporwa vitu vyao ambapo shule hizo ni shule ya msingi ya Kitunda na Jitihada, KC ya Saranga wamefanikiwa kugeuza kilabu cha pombe kuwa kikundi cha kijamii , KC ya Majohe wameweza kushirikiana na wananchi kutengeneza barabara iliyokuwa haipitiki kwa mud mrefu na KC ya Makurumla wameweza kuzibua mabomba yaliyokuwa yameziba ambapo yameanza kutoa maji.
Katibu wa Kituo cha taarifa na Maarifa cha Muzye, Josia Mahwa akitolea ufafanuzi kuhusu Vituo vya taarifa na Maarifa mkoa wa Kigoma wameweza kuhamasisha ujenzi wa nyumba za wahudumu ili kupunguza vifo vya mama na mtoto katika kata ya Muzye wakati wa kujifungua mabapo mwanzo kulikuwa na changamoto ya kibali kupitia kwenye mtendaji wa Mtaa au kiongozi wa Mtaa na kata ambapo wameweza kupata ushirikiano kupitia wananchi na uongozi wa Kata.
Mwenyekiti wa Kamati ya Wanawake na Uongozi kituo cha Taarifa na maarifa cha Mamire, Joyce Eliasi akitolea ufafanuzi kuhusu Vituo vya taarifa na Maarifa mkoa wa Manyara kwenye kituo vya taarifa na Maarifa cha Mamire waliweza kushawishi ujenzi wa mabweni ya wanafunzi wa kidato chaTano pamoja na kutoa elimu ya kupinga ukatili wa Kijinsia kupitia mikutano ya Vijiji na Vitongoji ambapo jamii imepokea elimu na kutoa taarifa ya ukatili unaofanyika dhidi ya watoto na wanawake kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali ikiwemo Mtadano wa Jinsia Tanzania (TGNP), Dawati la Jinsia la Wilaya, Ustawi wa jamii wa Wilaya, Watendaji wa Vijiji, PELUM Tanzania, Mother and Father Champion na COSITA
Katibu msaidizi wa Kituo cha taarifa na Maarifa cha Mkunwa, Laisa Mpingo akitolea uafanuzi kuhusu Vituo vya taarifa na Maarifa mkoa wa Mtwara wamefanikiwa kutatua changamoto ya ndia za utotoni kwa kuwashirikisha watendaji na viongozi wa vijiji pamoja na wanafamilia kwa kutoa elimu ili kuweza kupunguza changamoto hiyo kwenye jamii ambapo waliweza kuvunja ndoa ya mtoto mwenye umri wa miaka 15 kwa kushirikiana na mratibu wa Dawati la Jinsia
Mwenyekiti wawa Kituo cha taarifa na Maarifa cha Zilai, Joyce Mdoe akitolea maelezo kuhusu Vituo vya taarifa na Maarifa mkoa wa Tanga vilivyoweza kutatua changamoto ya kichomea taka katika zahanati ya Zirai ambayo iko karibu na shule ya msingi Zirai ambapo mwanzo moshi ulikuwa unaleta tatizo katika shule hiyo pamoja na kupatikana kwa manesi wawili katika Kituo hicho ili kutatua changamoto kipindi cha kujifungua kwa mama wajawazito na pia wameweza kumsaidia mwanafunzi ambaye hakuwa na uwezo wa kuendelea na masomo kwasababu ya kutokea familia duni.
Mkuruzenzi wa Shirika la Builders of Future Africa, Elisante Ephrahim akitoa maelezo kutoka Vituo vya taarifa na Maarifa mkoa wa Kilimanjaro kuwa kulikuwa na uchakavu wa Madarasa na mengine yalikuwa yadondoka katika wilaya ya Same hivyo waliweza kuchukua Taarifa sahihi na kuzipeleka sehemu husikakwa ajili ya kuweza kutatuliwa kwa haraka ambapo waliweza waliweza kupata pesa za Covid zilizopelekea ujenzi wa Madarasa 7 pamoja na kugawa taulo za kike kwa ajili ya wanafunzi kujistili wanapokuwa shuleni.
Mhasibu wa Kituo cha Taarifa na maarifa cha Ijombe, Scola Shaban kitoa ufafanuzi kuhusu Vituo vya taarifa na Maarifa mkoa wa Mbeya walikuwa na Bunge la jamii tarehe 14/06/2023 dambapo walifanya katika wilaya kwa kata zote nane katika KC Ijombe mkoa wa Mbeya ambapo wadau walioalikwa ni Diwani, Afisa Maendeleo, Watendaji wa Kata, Mwenyekiti wa Kijiji na wajumbe ambapo waliweza kufanya harambee ya mchango wa fedha kwa ajili ya kununua mabati ya kujengea Ofisi za Kijiji na ujenzi wa mabweni ya wasichana katika Sekondari ya Iwalanje na mpaka sasa ujenzi unaendelea.
Katibu wa Kituo cha Taarifa na maarifa cha Mngazi, Sinahamu Swala akitoa ufafanuzi kuhusu Vituo vya taarifa na Maarifa mkoa wa Morogoro wamefanikiwa kuibua mtoto aliyebakwa na shemeji yake ambapo waliweza kutoa taarifa na mtumiwa kukapatwa na sasa anashikiriwa na jeshi la polisi ambapo walitumia mbinu z kutoa taarifa kwa Mtendaji wa kijiji na kutupia askari wa kijiji ili kumkamata mtuhumiwa lakini changamoto walizopata ni kutopata ushirikiano kwa ndugu lakini wadau walioshirikisna na vituo hivyo ni Mtendaji wa Kijiji, Mtendaji wa Mtaa, Polisi kata na Daktari.
Mratibu wa Vituo vya Taarifa na maarifa Mkoa wa Mara, Paschal Elisha akitolea ufafanui kuhusu Vituo vya taarifa na Maarifa mkoa wa Mara wameweza kufanya ushawishi kwa wanajamii juu ya Ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Kata ya Regicheri, kuhamashisha wananchi katika ujenzi wa Shule ya mpya ya Msingi Rebu iliyoko wilaya ya Tarime Mjini, kuanzisha madawati ya Ulinzi na Usalama wa mtoto yapatayo 15 ngazi ya Sekondari na Msingi katika Wilaya ya Bunda na Musoma, unanzishwaji wa vyumba maalum vya wasichana kwenye shule za Sekondari 12,uanzishaji wa Zahanati ya kijiji cha Sombanyasoka pamoja na kuweza kuokoa mabinti zaidi ya 793 kuanzia mwaka 2016 hadi 2022 katika ukeketaji.
Katibu wa Kituo cha Taarifa na maarifa cha Kishapu, Robert Majembele akitoa ufafanuzi kuhusu Vituo vya taarifa na Maarifa mkoa wa Shinyanga vilivyoweza kujitolea kuchimba mashimo ya vyoo katika shule ambapo mpaka sasa mashimo hayo yamekamilika na boma limekamilika lenye matundu Saba hii ikiwani kupitia uraghabishi ikiwemo wana Kituo kuchimba wenyewe ili kuweza kutatua changamoto zilizopo kwenye jamii inayowazunguka.
Katibu wa Kituo cha Taarifa na maarifa cha Haubi, Anna Ambroseakitolea ufafanuzi kuhusu Vituo vya taarifa na Maarifa mkoa wa Dodoma wamefanikisha kuhamasisha ujenzi wa madarasa saba na matundu ya vyoo ambapo mwanzo shule iliyopo kwenye kijiji cha Ntomoko na pia katika kijiji cha Mafai imejengwa hospitali kwa nguvu ya wananchi kwa kushirikiana na Serikali ya kijiji ambapo mwanzo kulikuwa na changamoto wodi ya wajawazito ili kupunguza vifo vya mama na mtoto.
Baadhi ya washiriki kutoka vituo vya Taarifa na maarifa pamoja na asasi za kiraia wakichangia mada kwenye mafunzo ya ya Bajeti yenye mrengo wa kijinsia na ufuatiliaji wa vituo vya Taarifa na maarifa pamoja na asasi za kiraia.
Baadhi ya washiriki kutoka vituo vya Taarifa na maarifa pamoja na asasi za kiraia wakifuatilia mada kutoka kwa wataalam wa TGNP kwenye mafunzo ya siku mbili ya Bajeti yenye mrengo wa kijinsia na ufuatiliaji wa vituo vya Taarifa na maarifa pamoja na asasi za kiraia.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...