Dkt. Ladislaus Chang’a, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi, akizungumza wakati wa Warsha ya mafunzo kwa Wanahabari kuhusu Msimu wa Mvua za Vuli 2023, iliyofanyika leo Agosti 23, 2023 Kibaha Mkoani Pwani.
Afisa Uhusiano TMA, Monica Mutoni akifafanua wakati wa Warsha ya mafunzo kwa Wanahabari kuhusu Msimu wa Mvua za Vuli 2023, iliyofanyika leo Agosti 23, 2023 Kibaha Mkoani Pwani.



Baadhi ya waandishi wa habari wakisikiliza mada.
Picha ya Pamoja.

Na Karama Kenyunko Michuzi TV
VYOMBO vya habari nchini vimeshauriwa kuisaidia mamlaka ya haki ya hewa TMA kutoa taarifa sahihi za utabiri wa hali ya hewa kwa wakati ili kuweza kupanga na kutekeleza shughuli za kiuchumi na kijamii ikiwemo Kilimo kwa tija na ufanisi zaidi.

“Msimu unaokuja wa mvua za Vuli Oktoba hadi Disemba ni miongoni mwa misimu muhimu ya kilimo katika baadhi ya maeneo hapa nchini, hivyo ni muhimu kwa wananchi na watumiaji kupata taarifa sahihi na kwa wakati ili kuweza kupanga na kutekeleza shughuli za kiuchumi na kijamii ikiwemo Kilimo kwa tija na ufanisi zaidi.

Hayo yamesemwa leo Agosti 23, 2023 na Dkt. Ladislaus Chang’a, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi, wakati wa Warsha ya mafunzo kwa Wanahabari kuhusu Msimu wa Mvua za Vuli 2023.

Amesema msimu ujao wa mvua wa Oktoba hadi Disemba 2023 utachagizwa na uwepo wa El Nino ambayo ni hali ya kuongezeka kwa joto la uso wa bahari kwa eneo la kitropiki la kati ya Bahari ya Pasifiki, hali hiyo husababisha kuongezeka kwa viwango vya mvua na joto kwa baadhi ya maeneo hapa nchini, hivyo kufanya msimu wa mvua kuwa ni miongoni mwa misimu muhimu ya kilimo hapa nchini hususani maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka.

Dkt. Chang’a amesema serikali imeendelea kuijengea uwezo TMA na kuifanya iendelee kuimarisha huduma ikiwemo utoaji wa taarifa hizo kuwafikia watumiaji kwa wakati na kufanya maamuzi sahihi kwa wakati muafaka.

"Mamlaka inatarajia kutoa rasmi utabiri wa msimu wa mvua za Vuli 2023 kupitia vyombo vya habari, kesho siku ya Alhamis, saa 5:00 asubuhi, " amesema.

Pia aliwashukuru wanahabari kwa kuitikia mwaliko wa kuhudhuria warsha na aliwakumbusha kuendelea kuwa mabalozi wa TMA kwa jamii kwa kuimarisha usambazaji wa taarifa za utabiri na tahadhari.

TMA imekuwa na utaratibu wa kuandaa mafunzo ya kuwajengea uwezo wanahabari hususani wakati wa maandalizi ya utabiri wa mvua za msimu, ambapo wanahabari hao wanapata fursa ya kujadili na kupata ufafanuzi wa masuala mbalimbali kuhusiana na msimu husika.

Aidha, Dkt. Chang’a alieleza awali kuwa Serikali imeendelea kuijengea uwezo TMA na kuifanya iendelee kuimnarisha huduma ikiwemo utoaji wa taarifa hizo kuwafikia watumiaji kwa wakati na kufanya maamuzi sahihi kwa wakati muafaka.

Akihitimisha hotuba yake Dkt. Chang’a aliwashukuru wanahabari kwa kuitikia mwaliko wa kuhudhuria warsha na aliwakumbusha kuendelea kuwa mabalozi wa TMA kwa jamii kwa kuimarisha usambazaji wa taarifa za utabiri na tahadhari.

TMA imekuwa na utaratibu wa kuandaa mafunzo ya kuwajengea uwezo wanahabari hususani wakati wa maandalizi ya utabiri wa mvua za msimu, ambapo wanahabari hao wanapata fursa ya kujadili na kupata ufafanuzi wa masuala mbalimbali kuhusiana na msimu husika. Mamlaka inatarajia kutoa rasmi utabiri wa msimu wa mvua za Vuli 2023 kupitia vyombo vya habari, siku ya Alhamis, saa 5:00 asubuhi, tarehe Agosti 24, 2023.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...