MKURUGENZI wa kampuni ya Active Mama, Ernestina Mwenda maarufu kama ‘Coconut lady’ amewataka wakina mama kutumia vizuri mitandao ya kijamii kwa ajili ya kutengeneza fursa za kibiashara na kuachana na kutegemea fedha za kupewa.
Akizungumza na Michuziblog ameeleza namna gani wakina mama wengi wamekuwa wanavipaji, kama kusuka, kushona na vipaji vingine lakini hawataki kuvionesha kwenye mitandao ya kijamii na badala yake wanaonesha vitu vingine ambavyo sio vya muhimu.
Erestina amefunguka na kusema kuwa wakati alipoanza biashara ya kutengeneza mafuta ya nazi kupitia kampuni yake ya Active Mama, alikuwa hana mteja hata mmoja wa kumuuzia lakini alikuja kuwapata kupitia mitandao ya kijamii.
Kwa sasa amekuwa akimiliki biashara nyingi lakini msingi mkubwa ni mitandao ya kijamii, ambayo ndiyo wanamfanya kuongeza bidhaa kutokana na mahitaji ya wateja wake.
“Wakiongeza nguvu kwenye mitandao ya kijamii, kila mwanamke anauwezo wa kutengeneza kiasi kikubwa cha fedha.
Anasema anapenda kuitwa Coconut Lady kwakuwa anaamini nazi ndiyo maisha yake na maisha yake ni nazi, sababu maisha yake ya ujasilia mali yalianzia katika utengenezaji wa mafuta ya nazi.
Anasema ingawa sasa amekuwa na biashara nyingi kama Siagi, sabuni, unga wa lishe na unga wa mbegu za maboga, lakini vyote hivyo alivipata baada ya utumia mitandao ya kijamii kama sehemu ya kujitangaza.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...