NA
K-VIS BLOG, NJOMBE
Waziri
wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana ametembeklea banda
la Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakzi (WCF) kwenye Tamasha la pili la kitaifa la Utamaduni
linaloendelea katika viwanja vya Stendi ya zamani mkoani Njombe.
WCF
ni miongoni mwa Taasisi mbalimbali za serikali zinazoshiriki ili kutoa huduma
kwa wananchi na wadau mbalimbali waliokusanyika kutoka mikoa mbalimbali nchini
ikiwemo ile ya Nyanda za Juu Kusini.
Akiwa
kwenye banda hilo, Mhe. Dkt. Chana, alipata fursa ya kupewa elimu ya Fidia kwa
Wafanyakazi iliyokuwa ikitolewa na Afisa Madai Mwandamizi wa WCF, Bi. Asia
Jingu.
Alijulishwa
kuwa WCF inatoa fidia endapo mfanyakazi ataumia au kuugua kutokana na kazi na
endapo atafariki basi wategemezi wake watalipwa fidia.
Pia
alielezwa kuwa Mfuko uliundwa kwa mujibu wa Kifungu cha 5 cha Sheria ya Fidia
kwa Wafanyakazi [Sura 263 marejeo ya mwaka 2015] na inahusu waajiri na
waajiriwa wote kutoka sekta ya umma na binafsi Tanzania Bara.
Aidha
Mhe, Waziri ambaye alifuatana na Mkuu wa Wilaya ya Nkombe ambaye alikuwa anakaimu nafasi ya Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Kissa Gwakisa Kasongwa alielezwa kuwa Mfuko unatoa jumla ya Mafao saba ambayo ni pamoja na
Huduma ya matibabu, Malipo ya ulemavu wa muda, Malipo ya ulemavu wa kudumu,
Malipo kwa anayemhudumia mgonjwa, Huduma za utengemao, Msaada wa mazishi na
Malipo kwa wategemezi endapo mfanyakazi atafariki.
Tamasha hilo la Kitaifa linalofanyika mkoani humo linaongozwa na kaulimbiu inayosema “Utamaduni ni Msingi wa maadili tuulinde na kuuendeleza”.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...