Mfuko wa Ruzuku wa Wanawake Tanzania (WFT-Trust) umeendesha Mkutano wa Jamii kwa ajili ya kupitia matokeo ya utafiti ambayo yamefanyika ndani ya miaka miwili katika Kata 18 wilayani Shinyanga, na kubainishwa mbinu Saba za kutokomeza ukatili wa kijinsia ndani ya jamii.
Mkutano uliohusisha, viongozi mbalimbali wa Serikali, pamoja na wanamabadiliko ngazi ya jamii (backbone) na Mabaraza ya watoto.

Mkuu wa Idara ya ukuzaji Rasilimali na Mawasiliano kutoka (WFT-Trust) Carol Mango, amesema utafiti huo umefanyika kwa mudawa miaka miwili kuanzia 2021 hadi 2023kwa kushirikiana na Shirika la Citizens for Change ambao ndiyo walikuwa watekelezaji wa utafiti,na WFT ni watoaji wa Ruzuku.

Naye Mathias Mkude kutoka Citizen for Change na TICD akiwasilisha matokeo ya utafiti, amesema katika utafiti huo wahusika wenyewe ambao ni wanabadiliko ngazi ya jamii (Backbone) walitengeneza mbinu saba ambazo zitasaidia kutokomeza ukatili wa kijinsia, kuwa ni kufufua vikao vya familia nyakati za usiku (Shikome) ambavyo licha ya kuzungumza vikao vya familia pia vitatumika katika mazungumzo ya kupinga ukatili.

Mkude ametaja Mbinu zingine kuwa ni kuhamasisha viongozi na Walimu Wakuu kuelimisha walimu kuhusu masuala ya ukatili, kuhamasisha viongozi wanawake na watoto kuhudhuria kwenye Mikutano ya kijiji na kutoa maoni yao dhidi ya kupambana na vitendo vya ukatili.

Pia kupitia Mikutano hiyo itumike kupitisha Sheria ndogo ambazo zitasaidia kupambana na ukatili, kushawishi viongozi wa Kata na vijiji kutoa adhabu kali kwa watu ambao wanaendekeza ukatili, kuwezesha midahalo ya kijamii kujadili namna ya kuzuia ukatili, pamoja na kutungwa sheria kali kwa wazazi ambao wanabagua watoto na kutowapeleka shule.

Naye Carol Mango, amesema kupitia utafiti huo pia wamebaini kwamba mifumo isiyo rasmi imekuwa ikiamika sana na jamii katika kupambana na ukatili na ndiyo wamekuwa wakipewa taarifa za ukatili tofauti na mifumo ambayo ni rasmi ambao wao ndiyo watoa maamuzi.

“Lengo la utafiti huu ni kujifunza pamoja na kuishirikisha jamii na kuwa na nguvu ya pamoja na kubaini mbinu ambazo zinaweza kutumia katika kukabiliana na matukio ya ukatili wa kijinsia ndani ya jamii,”amesema Mango.

Afisa Mipango kutoka WFT Neema Msangi, amesema mradi huo wa utafiti wameufanya katika Mkoa wa Shinyanga, sababu ni mkoa ambao ukatili wa kijinsia upo juu, na wakajielekeza katika wilaya ya Shinyanga na kutoa Ruzuku kwa wadau mbalimbali ili kufanya shughuli za kutokomeza ukatili ndani ya jamii.

Mgeni rasmi katika Mkutano huo ambayr ni Diwani wa Kata ya Itwangi Sonya Jilala Mhela, ameipongeza WFT kwa mradi huo wa utafiti ambao wameufanya na umesaidia kwa kiasi kikubwa kuibadilisha jamii juu ya masuala ya ukatili sababu elimu ya kupinga ukatili wa kijisia imeyafikia makundi yote.
Mkuu wa Idara ya ukuzaji Rasilimali na Mawasiliano kutoka (WFT-Trust) Carol Mango.
Mathias Mkude kutoka Citizen for Change na TICD
Afisa Mipango kutoka WFT-Trust Neema Msangi.
Mratibu wa WFT-Trust Mkoa wa Shinyanga Glory Mbia akizungumza kwenye Mkutano huo.


Wajumbe wakiwa kwenye Mkutano.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...