MUHUBIRI wa Kimataifa kutoka nchini Nigeria kuliombea Taifa la Tanzania mkutano unaotarajiwa kufanyika mapema Mwezi Oktober 2023 Ubungo plaza Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza Leo Septemba 15,2023 Jijini Dar es Salaam Mratibu wa mkutano huo wa kuliombea taifa mtumishi Addo November Mwasongwe amesema Mkutano huo utaanza rasmi octoba 18 hadi 22,2023 ambapo Muhubiri wa Kimataifa kutoka nchini Nigeria Apostle Arome akishirikiana na wahubiri wengine nchini Tanzania.

"Tunafahamu kazi kubwa anayofanya Rais Mama Sami kuhakikisha Tanzania inakuwa nchi ya Amani na yenye uwekezaji wenye tija hivyo sisi kama viongozi wa dini tunajukumu la Kumuombea Rais wetu pamoja na Taifa kwa ujumla amani iendelee ili tupate wawekezaji wengi nchini kwetu na pato la taifa liimarike na kuongezeka".

Novemba ameeleza kuwa mkutano huo hautakuwa na kiingilio badala yake washiriki wote wanatakiwa kuwasilisha maombi yao mapema kupitia mitandao ya kijamii au kutumia namba ya simu.

"Mkutano huo wa Injili wa kimaombi wa kuombea Taifa watanzania wanatakiwa kujiandikisha kwa kutuma ujumbe wa maandishi au watsap kwenda namba 0718500000 kujisajili ambapo hakutakua na kiingilio japo kujiandikisha ni lazima".

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...