Na Muhidin Amri, Tunduru

CHAMA Kikuu cha Ushirika wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma (Tamcu Ltd),kimenunua maghala mawili yenye uwezo wa kuhifadhi zaidi ya tani 5,000  za mazao ya wakulima wanaohudumia na Chama hicho.

Meneja Mkuu wa Tamcu Imani Kalembo alisema hayo jana, kwa wajumbe wa mkutano Mkuu maalum uliofanyika katika ukumbi wa Skya Way Tunduru mjini.

Alisema,kwenye maghala hayo kuna mizani kubwa yenye uwezo wa kupima magari,majengo ya ofisi na huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo vyoo.

Alisema,wamepokea taarifa kutoka kwa kamishina wa ardhi mkoa wa Ruvuma ikithibitisha uhalali wa mmiliki wake na kuongeza kuwa majengo hayo yanaweza kununuliwa kwa bei ya juu Sh.milioni 546,063,378 na bei ya chini Sh.milioni 464,100,000.

Aidha  Kalembo alisema,baada ya majadiliano  ya muda mrefu muuzaji ambaye ni mmiliki wa maghala hayo amekubali kuuza kwa bei ya Sh.milioni 492,000,000.

Kalembo amewapongeza wanachama wa Tamcu ambao kupitia Mkutano Mkuu maalum,wameridhia kununua maghala hayo ambayo yatakuwa sehemu ya vyanzo vikubwa vya mapato kwa Chama Kikuu.

Mwenyekiti wa Tamcu Mussa Manjaule alisema,malengo ya chama hicho ni kuendelea maghala mengi zaidi kwa ajili ya kuhifadhi mazao ya wanachama ambapo kwa sasa wanalazimika kukodi maghala ya watu binafsi kwa gharama kubwa.

Manjaule alisema,wilaya ya Tunduru kupitia Chama kikuu cha Ushirika(Tamcu Ltd) inafanya vizuri na kupata sifa kutokana na kuendesha shughuli za Ushirika kwa haki na kuwataka viongozi wa vyama vya msingi(Amcos)kusimamia ushirika na kuwasaidia wanachama kuongeza uzalishaji wa mazao.

Mkuu wa wilaya ya Tunduru Julius Mtatiro,amewapongeza viongozi wa Amcos na Tamcu kwa mipango mizuri ambayo itasaidia kuongeza mapato yatakayowezesha kuimarisha vyama vya Ushirika.

Hata hivyo,amewataka kuwa waadilifu na waaminifu katika shughuli zao ili kuepuka malalamiko kutoka kwa wanachama na kuzalisha migogoro inayoweza kuvuruga shughuli za usimamizi  na uendeshaji wa Ushirika.

“viongozi mkifanya mambo mazuri mtaendelea kukumbukwa daima hata baada ya kuondoka madarakani,hivyo nawaomba  wasaidieni wanachama wenu ambao bado wanahitaji msaada wenu ili waweze kuondokana na umaskini kupitia shughuli zao za kilimo”alisema Mtatiro.

Mtatiro,amewaagiza viongozi wa Amcos,kwenda kuhamasisha wakulima kuongeza kiwango cha uzalishaji wa maarufu la mbaazi ambalo kwa sasa limekuwa kati ya mazao yenye mchango mkubwa kwa uchumi na maendeleo ya wananchi wa wilaya ya Tunduru

Meneja masoko wa Tamcu Marcelino Mrope wa  tatu kushoto,akiwaonyesha baadhi ya wajumbe wa bodi ya Tamcu wakiongozwa na Mwenyekiti wake Mussa Manjaule wa kwanza kushoto maghala  mawili yaliyonunuliwa na Chama hicho kwa ajili ya kuhifadhi mazao ya wakulima.
Maghala mawili yaliyonunuliwa na Tamcu kwa ajili ya kuhifadhi mazao ya wakulima ambao ni wanachama wa Tamcu.
 Baadhi ya wajumbe wa mkutano mkuu maalum wa Chama kikuu cha Ushirika(Tamcu Ltd)wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Tunduru wakili Julius Mtatiro(hayupo pichani).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...