Kampuni ya Sukari Kilombero (KSCL) imechangia katika safari ya elimu ya muogeleaji mahiri, Collins Saliboko kwa kutoa kiasi cha dola za Kimarekani 5,000 kama sehemu ya ada ya kozi ya Usimamizi wa Michezo katika Chuo Kikuu cha Indianapolis, Marekani.

Hafla fupi ya makabidhiano ilifanyika tarehe 25 Agosti katika ofisi za Kampuni jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Mkurugenzi wa Biashara, Fimbo Butallah. Katika hafla hiyo, Bwn. Butallah, alikabidhi hundi ya mfano kwa Collins Saliboko, kuashiria dhamira ya kampuni ya kumsaidia kufikia malengo yake ya elimu.

Uamuzi wa Kampuni kumsaidia Collins Saliboko ni mfano wa namna ambayo kampuni zinaweza kusaidia vijana wenye vipaji na kuchangia katika utengenezaji wa fursa za ajira na kujiajiri. Mchango wa KSCL katika safari ya elimu ya Collins Saliboko unathibitisha dhamira ya kampuni katika kuwekeza kwenye kuwawezesha vijana, kukuza uongozi, na kukuza ujuzi kama baadhi ya mikakati ya kuleta mabadiliko chanya katika jamii kwa ujumla.

Kampuni ya Sukari Kilombero (KSCL) imechangia katika safari ya elimu ya muogeleaji mahiri, Collins Saliboko (kulia) kwa kutoa kiasi cha dola za Kimarekani 5,000 kama sehemu ya ada ya kozi ya Usimamizi wa Michezo katika Chuo Kikuu cha Indianapolis, Marekani. Hafla fupi ya makabidhiano ilifanyika tarehe 25 Agosti katika ofisi za Kampuni jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Mkurugenzi wa Biashara, Fimbo Butallah (kushoto).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...