Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Chalinze Islamic Modern, Bagamoyo Mkoani Pwani, wameiomba Serikali kuelekeza nguvu katika ujenzi wa maabara za masomo ya sayansi kuanzia elimu ya msingi ili kuwapa uelewa wa masomo ya sayansi kwa vitendo .
Wameeleza, zipo Shule za msingi ambazo zina wanafunzi wenye uwezo wa kufanya sayansi ya vitendo changamoto ikiwa ni ukosefu wa vifaa.
Ushauri huo umetolewa na wanafunzi wa darasa la sita katika shule Msingi Chalinze , Islamic Modern baada ya wanafunzi hao kumfanyia upasuaji mnyama Sungura na kumrejesha hai.
Wanafunzi hao walieleza,licha ya masomo ya kawaida pia wanapatiwa mafunzo ya sayansi, na kwamba tukio la hilo ni kiumbe wa tatu kumfanyia upasuaji huo.
Wanafunzi Lattifa Bakari na Mussa Swed wa darasa la sita walieleza,wamefanikiwa kuwafanyia upasuaji viumbe hao ambao wote wamefanikiwa na wapo hai.
Nae Swed alisema, Tanzania ina uhaba wa madaktari bingwa hivyo kwa kuandaa wanafunzi wa sayansi kuanzia ngazi ya msingi itakuwa na uwekezaji mkubwa wa kizazi cha madaktari hao.
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu Seif Hashimu alisema ,shule yao imeamua kuwapatia masomo ya sayansi wanafunzi wao kwa lengo la kuwajengea uwezo ili waendapo sekondari wasiwe wageni kwenye somo hilo.
Mwalimu Issa Machame alisema kuwa wanafundisha masomo hayo kwa lengo la kuwapatia taaluma hiyo wanafunzi wanaoanzia elimu ya msingi, ili hata watakapoingia sekondari wakikutana na masomo hayo wasiyaone mageni.
Home
HABARI
MAABARA ZA MASOMO YA SAYANSI ZIANZIE NGAZI YA ELIMU YA MSINGI ILI KUANDAA MADAKTARI BINGWA WA BAADAE
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...